Kubenea hana imani na polisi
DAR ES SALAAM
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea jana alidai kuwa haliamini Jeshi la Polisi katika uchunguzi kwa matukio yanayokihusu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Kubenea alitoa madai hayo jana Dar es Salaam kwa kueleza kuwa polisi wamekosa sifa na hawaaminiki tena.
Alidai kusikitishwa na polisi kwa sababu wanavunja sheria za nchi.