Dk. Kijo-Bisimba atakiwa kupima kauli zake

Date:

Share post:

Dk. Kijo-Bisimba atakiwa kupima kauli zake

DAR ES SALAAM

UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umemtaka Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba kupima kauli zake za kuishutumu Serikali kwa sababu haziendani na umri wake.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka ndiye aliyetoa kauli hiyo jana alipokuwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC.
Katika mahojiano hayo, Shaka alisema huenda Dk. Bisimba amefurahishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka damu imwagike au yatokee mauaji kama  ya Misri na Libya.
Shaka alisema anaamini Dk. Bisimba ni msomi mwenye upeo, mchambuzi hodari na mtetezi wa masuala ya kisheria hivyo hapaswi kufumbia macho kauli za Mbowe.
“Mama yetu nadhani  sasa ameanza kuzeeka. Amepoteza uwezo wake mkubwa wa kupambanua mambo kwa kutazama haki na usawa. Nasita kumwita mshabiki badala ya kuwa mtumishi bora wa jamii.
“Tunafahamu  kituo cha sheria kimekuwa kikitumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa kuendesha mikutano ya kiharakati , kishinikiza mapambano dhidi ya Serikali pia mara kadhaa kutaka kukivuruga chama tawala. Tumewatambua na katu hatutawaonea aibu,” alisema Shaka.
Alimtaka Dk Bisimba kueleza uhuru mpana  wa vyombo vya habari uliopo nchini unapatikana sehemu gani katika Bara la Afrika hata atamke umepotea nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...