Wednesday, December 25, 2024
spot_img

KAKONKO WAOMBA WATAALAM WA MIAMBA

MACHI 2, 2018
KAKONKO WAOMBA WATAALAM WA MIAMBA
Naibu Waziri   wa   Madini,   Stanslaus   Nyongo 
KAKONKO
Wananchi   wa   Wilaya   ya   Kakonko,   mkoani   Kigoma   wameiomba Serikali isaidie kuwapatia wataalam wa miamba watakaotafiti na kubainisha kiasi  cha   madini   yaliyogundulika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.
Akiwasilisha taarifa ya wilaya kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus   Nyongo ambaye yuko katika ziara ya kikazi wilayani humo, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala alisema Madini ya Dhahabu yamegundulika katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Alitaja baadhi ya maeneo yaliyogundulika kuwa na madini hayo ni pamoja na Nyamtukuza, Kasuga na Muhange lakini haijaweza kufahamika ni kiasi gani kilichopo.
“Tunakuomba   utusaidie   upatikanaji   wa   wataalamu   ili   kujuata kwimu sahihi za kiasi cha madini kilichopo kwenye maeneo yaliyogundulika,” alisema.
Kanali Ndagala alisema wilaya hiyo ina madini mengi chokaa katika Hifadhi   ya   Pori   la   Akiba   la   Moyowosi   lakini hayachimbwi kwa sababu ya sheria za hifadhi haziruhusu.
Akijibu maombi hayo, Naibu Waziri Nyongo alisema Serikali itafanya tafiti mbalimbaliza madini nchini kwa kuwatumia wataalamu wa jiolojia kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST).
 “Tutawaelekeza wataalam wetu wafike hapa Kakonko kufanya utafiti,” alisema Nyongo.
Aidha, aliahidi kulifanyia kazi suala la upatikanaji wa Madini ya Chokaa katika eneo la hifadhi.
Naibu   Waziri   Nyongo,   anaendelea   na   ziara   yake   ambayo itahitimishwa mkoani Kigoma baada ya kuitembelea mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera.

Naibu   Waziri   wa   Madini,   Stanslaus   Nyongo   (wa   nne   kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kakonko.

Naibu   Waziri   wa   Madini,   Stanslaus   Nyongo   akizungumza   na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kakonko, ofisini kwa mkuu wa wilaya hiyo jana.



Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya