MACHI 3, 2018
ZITTO AZIDI KUACHWA
![]() |
| Zitto Kabwe |
DAR ES SALAAM
Taarifa zilizotufikia kutoka Kata ya Gehandu, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara zinaeleza kuwa Diwani ya Chama cha ACT-Wazalendo wa kata hiyo, Mathayo Samhenda, amejiuzulu udiwani na kujivua uanachama wa chama chake muda mfupi uliopita.
Zimeeleza kuwa diwani huyo baada ya kujiuzulu na kujivua uanachama wa ACT- Wazalendo ametangaza kujiunga na CCM.
Taarifa kutoka Hanang zimeeleza kuwa kujiuzulu kwa diwani huyo kumekuja ikiwa ni siku chache baada ya kumkabili ana kwa ana Kiongozi wa chama, Zitto Kabwe na kumweleza kutoridhika na mwenendo wa mambo ndani hicho hivyo anakusudia kukipa kisogo.
Zitto alikabiliwa na diwani huyo Februari 27, mwaka huu kwenye kikao cha ndani kilichofanyika wilayani Hanang inakodaiwa kuwa Zitto alimfukuza Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo wa Mkoa wa Manyara.







