SERIKALI YATUMIA BILIONI 58 KUKAMILISHA MIRADI YA MAJI UKEREWE

Date:

Share post:

 

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imekamilisha ukarabati na upanuzi wa miradi ya maji katika Wilaya ya Nansio mkoani Mwanza kwa gharama ya sh bilioni 58.

Hayo yameelezwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa Nansio jana katika uwanja wa Getrude Mongela.

Majaliwa ambaye yuko katika ziara ya kisiasa nchi nzima ya kumnadi mgombea urais wa CCM, Rais John Pombe Magufuli, amesema kati ya fedha hizo, sh bilioni 13 zimetolewa kwa ajili ya miradi ya maji ikiwemo sh bilioni 10.9 za uboreshaji wa huduma ya maji safi mjini Nansio utakaonufaisha wananchi 108,653.

Amesema sh bilioni 2.1 zimetumika kwa ajili ya kuboresha huduma ya usafi wa mazingira  mjini Nansio.

Ameitaja miradi mingine ya maji iliyokamilishwa na Serikali ya Rais Magufuli kwa gharama ya sh bilioni 1.3 kuwa ni ukarabati wa mradi wa maji wa Irugwa, mradi wa maji ya bomba ya Nansore, mradi wa maji wa Muriti/ Ihebo, upanuzi wa mradi wa maji wa Chabilungo na upanuzi na ukarabati wa mradi wa maji Kazilankanda

 

Previous article
Next article

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

JELA MIAKA 30 KWA KUPATIKANA NA BANGI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imemhukumu Brown Frank Mwaitubi (31), mkazi wa Kajunjumele, kifungo cha miaka...

DUTERTE KUPANDISHWA KIZIMBANI ICC

MANILA, Ufilipino JOPO la majaji watatu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) limethibitisha kuwa Rais wa zamani wa...

WRIGHT: RICE APEWE BALLON D’OR

LONDON, Uingereza MKONGWE wa Arsenal, Ian Wright, amemtaja Declan Rice kuwa anastahili kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka...

ISRAEL, LEBANON ZAONGEZA WIKI TATU ZA KUSITISHA VITA

WASHINGTON DC, Marekani RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema Israel na Lebanon zimekubaliana kuongeza wiki tatu za kusitisha mapigano. Wakati...