ZAIDI YA BILIONI 5 ZATUMIKA KUJENGA BARABARA YA NGARA

Date:

Share post:

 

NA MWANDISHI WETU

SHILINGI bilioni 5.26 zimetolewa kupitia Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara katika Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera.

 “Kati ya hizo, shilingi bilioni 1.1 zimetengeneza barabara kwa kiwango cha lami kilomita 4.5 katika makao makuu ya wilaya hii.”

Hayo yamesemwa leo (Jumatano, Septemba 30, 2020) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Rulenge, katika mikutano uliofanyika kwenye stendi ya Rulenge.

Amesema kiasi kingine cha shilingi bilioni 4.16 zimetolewa kupitia TARURA kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara ikiwemo barabara za Muhweza – Mukarehe, Keza – Nyanzovu, Mukalinzi – Mulonzi, Kibuba – Gwenzaza, Murugwanza – Runzenze (Airstrip), Chivu – Ntobeye – Nyakiziba,Buhororo – Mukididili, Ngara – Kumutana na Buhororo – Ruganzo (Airstrip)

Majaliwa ambaye leo anamalizia ziara yake mkoani Kagera ya kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ngara, Ndayisaba George Ruhoro na mgombea udiwani wa CCM wa kata ya Rulenge, John Niyonzima.

Mapema, akiwa njiani kuelekea Ngara akitokea Bukoba mjini, Majaliwa alisimamishwa na wakazi wa kata za Nyaishozi (Karagwe) na Kasulo Benaco (Ngara) ambako pia aliwanadi madiwani wa kata hizo. Pia aliwaeleza kwamba barabara ya kutoka Omurushaka hadi Benaco itajengwa kwa kiwango cha lami.

“Kwenye Ilani ya uchaguzi iliyopita ambayo inaisha sasa, barabara hii ilielezwa kwamba itakamilishwa kufanyiwa upembuzi yakinifu, na sasa inaenda kujengwa kwa lami kwa sababu kazi imeshafanyika.”

Pia aliitaja barabara nyingine ya kutoka Bugene – Kasulo (BENACO) yenye urefu wa km. 124 ambayo inatajwa kwenye uk. 75 wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwamba ni miongoni mwa barabara zitakazoanza kujengwa upya kwa kiwango cha lami.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS RAMAPHOSA ‘AMTUMBUA’ MKUU WA POLISI

PRETORIA, Afrika Kusini RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametengua uteuzi wa Mkuu wa Polisi nchini humo, Jenerali Fannie...

PAPA AKOSOA MATESO YA WAFUNGWA GUINEA

MALABO, Guinea ya Ikweta KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, ameeleza kutokuridhishwa na namna wafungwa wanavyoishi katika...

LEAO AINGIA RADA ZA UNITED, LIVERPOOL

MILAN, Italia MANCHESTER United na Liverpool zimeingia kwenye ushindani mkali wa kuiwania saini ya winga wa AC Milan, Rafael...

MAN CITY YATUA KWA ENZO WA CHELSEA

LONDON, Uingereza KLABU ya Manchester City inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, wakati wa usajili wa...