‘TFF KUGAWA NOTI NI KAWAIDA’

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA – 0711 46 49 84

IMEELEZWA kuwa Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) kuwagawia noti waandishi wa habari kila linapowaita kuandika Habari za shirikisho hilo ni utaratibu wake wa kawaida.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wanahabari waliojitokeza kueleza hisia zao baada ya kuripotiwa kuwa TFF imewamwagia mamilioni ya fedha wahariri wa michezo wa vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wanahabari aliyehudhuria mkutano wa Rais Karia na kupata mgao huo, Asha Muhaji akizungumza kwa hasira baada ya kutolewa kwa taarifa ya kuwepo kwa mgawo huo alisema amekasirika sana.

Akizungumza huku akitetemeka shingo, Muhaji amelaumu kuripotiwa kwa mgawo huo na kueleza kuwa ni utaratibu wa kawaida lakini haukupaswa kuwekwa hadharani.

“TFF kuwapa hela waandishi au wahariri bila kuwasainisha mahali popote ni utaratibu wao wa kawaida kwa zaidi ya miaka nane sasa. Hizo ni hela ndogo sana sema hujui kuwa inapokea Dola za Marekani nyingi kutoka FIFA na CAF na inaruhusiwa kuzitumia inavyoona inafaa.

“Kilichonikasirisha ni kusambazwa kwa taarifa ya wahariri kuhongwa. Hili jambo lilikuwa la siri sasa kwenda kuliweka public kuna maana gani kama siyo kuchafuana? Takukuru walishakagua sana hesabu za TFF, wanajua kuna pesa za waandishi ndiyo maana hujasikia kitu,” alisema Muhaji.

Kauli hiyo ya Muhaji iliungwa mkono na mwanahabari mwingine, Frolian Kaijage ambaye katika andiko lake kwenye group la wanamichezo la mtandaoni alieleza kuwa hizo ni fedha za mafuta.
“Hakika Asha, hizo ni fedha za ‘mafuta’ tulikuwa tukiziita hivyo nikiwa Afisa Habari pale Karume. Ni miaka takriban nane tangu nitoke pale na ninafikiri kiwango tulichokua tunatoa wakati ule hakina tofauti na hiki cha sasa,” aliandika Kaijage.

Afisa Habari wa TFF, Clliford Mario Ndimbo alipoulizwa kuhusu uhalali wa utaratibu huo alisema suala hilo hawezi kulizungumzia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...