Wednesday, December 25, 2024
spot_img

SIMBA, FISI WALISHWA SUMU

RIPOTA PANORAMA
SIMBA sita na Fisi zaidi ya 100 wamekufa baada ya kulishwa simu iliyowekwa kwenye nyama pembezoni mwa Hifadhi ya Ruaha.

Pamoja na wanyama hao, ndege zaidi 100 nao wamekufa baada ya kula mizoga ya Simba na Fisi iliyowekewa sumu na wafugaji, wiki tatu zilizopita.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalaah alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani yaliyofanyika mjini hapa leo.

Waziri Kigwangallah ameeleza kusitikishwa na mauaji hayo ya wanyama na ndege aliyoyaita kuwa ya kulipiza kisasi.

Ameonya kuwa Serikali itachukua hatua kali kwa watu wanaoua wanyama jamii ya paka wakubwa kwa sababu wapo katika hatari ya kutoweka.

Amesema wakati wanyama wa jamii ya paka wakubwa wakiwa katika hatari ya kutoweka, Faru na Tembo wamekuwa katika hatari hiyo kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa takwimu za Taasisi ya Wanyapori (Tawiri) Tanzania kuna Simba 16,800, Chui 25,000 na Duma 1180.

Biashara ya utalii hapa nchini inachangia asilimia 18 ya pato la Taifa na asilimia 25 ya fedha za kigeni huku akitoa ajira kwa watu 500,000 za moja kwa moja na ajira zisizokuwa za moja kwa moja zaidi ya milioni mbili.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya