MKANDARASI SOKO LA TANDALE MWIZI MDOGO MDOGO – MKURUGENZI KINONDONI

Date:

Share post:

 

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kinondoni, Aron Kigurumjuli

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, Aron Kigurumjuli amesema mkandarasi aliyepewa kandarasi ya kujenga soko jipya la Tandale, Namis Corporation LTD ni mwizi mdogo mdogo ambaye akikamatwa hurejesha alichoiba.

Kigurumjuli aliyasema hayo wiki iliyopita katika mahojiano maalumu na Tanzania PANORAMA Blog yaliyofanyikia Kinondoni Dar es Salaam.

Alikuwa akijibu kuhusu madai kuwa, mkandarasi huyo alighushi leseni yake ya biashara na alibainika kutenda kosa hilo wakati akisaka zabuni ya ujenzi wa soko la Tandale.

Katika majibu yake, Kigurumjuli alisema Namis Corporation LTD haikughushi leseni ya biashara isipokuwa ilifanya udanganyifu ulioiwezesha kuwa inalipa pesa kidogo kinyume na hitaji la leseni yake na hivyo ikawa inaiibia serikali pesa kidogo za tozo ya leseni.

Kigurumjuli alisema, wataalamu wake walibaini kuwepo kwa dosari hiyo kwenye leseni ya Namis Corporation LTD wakati wa ukaguzi wa nyaraka uliofanyika kabla ya kuzawadiwa zabuni ya ujenzi wa soko la Tandale.

“Unasema inadaiwa si ndiyo? sasa mimi nakwambia madai hayo ni uongo. Namis hajaghushi leseni ya biashara, sema, acha nikusaidie yule alikuwa akiiba kidogo hela za serikali. Ni mwizi mdogo mdogo tu lakini tulimbaini tukambana, akakiri tukampiga faini, akalipa.

“Alikuwa anaibaje, sikiliza. Leseni za biashara zipo za aina nyingi sana, zipo za mpaka Dola za Marekani 200,000. Huyu leseni yake alipaswa alipie kiwango cha juu lakini yeye akakataka ya kiwango cha chini, akawa analipa below ya kiwango anachopaswa kulipa. Kama sikosei kwa shughuli zake za ukandarasi alipaswa kulipa 60,000 lakini yeye akawa analipa 30,000.

” Sasa wakati wa ukaguzi wa nyaraka zake alipokuwa ameomba tenda ya soko la Tandale wataalamu wangu wakagundua huyu anatuibia, anaiibia serikali. Wakambana, alibishabisha kidogo lakini alibanwa haswa akakubali kulipa.

“Tulimpiga faini kubwa. Shilingi milioni nane ya miaka mitano aliyokuwa amefanya ujanja wake. Sasa huyu huwezi kumpa kosa kubwa hilo la kughushi, huyu ni mwizi mdogo mdogo tu na alibanwa akalipa. Hayo mengine sasa kamuilize mwenyewe,” alisema Kigurumjuli.

Tanzania PANORAMA Blog imemtafuta Mkurugenzi wa Namis Corporation LTD, Thomas Uiso kuzungumzia suala hilo bila mafanikio kwani tongu aliposema mambo yote yanayohusiana na kukwama kwa ujenzi wa soko jipya la Tandale ambalo yeye ndiye mkandarasi aulizwe Mkurugenzi Kigurumjuli amekuwa hapokei simu wala kujibu ujumbe wa maandishi.

Tanzania PANORAMA jana lilimpigia simu Uiso hakupokea na lilimtumia ujumbe wa maandishi kumuuliza kuhusu jambo hilo hakuujibu licha kuonyesha umemfikia na ameusoma.

Taarifa zilizolifikia Tanzania PANORAMA Blog zilieleza kuwa kampuni hiyo ulighushi leseni ya biashara na ilipata kandarasi mbalimbali kwa kutumia leseni hiyo ya kughushi.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...