WATUMISHI WAPYA WA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

Date:

Share post:

Watumishi wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mwananchi.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainabu Athman Katambi (Mb), wakati akifungua mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya 162 wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Lush Garden, mkoani Arusha.

Mhe. Katambi amesema watumishi hao wanapaswa kutumia taaluma zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Tunatarajia kuona watumishi waadilifu, wenye kufanya kazi kwa weledi na umahiri, wakizingatia misingi ya uadilifu na kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa haki kwa maslahi mapana ya Taifa,” amesema.

Aidha, amesisitiza kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni mhimili muhimu katika kusimamia utekelezaji wa haki nchini, hivyo kuna umuhimu wa kuimarisha taasisi hiyo ili iendelee kusimamia haki jinai kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka, Bw. Sylvester Mwakitalu, amesema waajiriwa hao wapya wanatarajiwa kufanya kazi katika ofisi za wilaya mbalimbali nchini, ambapo hadi sasa kuna ofisi 118 zilizoanzishwa kufuatia juhudi za Serikali za kuimarisha huduma za mashtaka.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya maadili ya utumishi wa umma na kuwapa uelewa wa kina kuhusu majukumu yao ya kila siku ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa haki.

Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha sekta ya sheria kwa kuhakikisha watumishi wake wanakuwa na weledi, ufanisi na wanazingatia misingi ya haki katika kuwahudumia wananchi.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...