WATEKAJI WATAKA MIL. 57/- KUMWACHIA MWANAFUNZI

Date:

Share post:

LAGOS, Nigeria

VIDEO iliyosambaa katika mitandao ya kijamii imemuonesha kijana aliyetajwa kuwa ni mwanafunzi akiomba kuokolewa, huku watekaji wakishinikiza walipwe kwanza Naira milioni 30 (zaidi ya Sh mil. 57 za Tanzania) ili kumwachia.

Kwa mujibu wa John Arum Azi mkazi wa Kaduna na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jo, alitekwa na watu wasiojulikana alipokuwa akirejea nyumbani na marafiki zake sita, ambao pia wanashikiliwa.

Taarifa zinaeleza kuwa watekaji walimlazimisha kijana huyo kujirekodi akiomba msaada, na kish kuposti kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook.

Watekaji wamesema wanaahitaji kulipwa Naira milioni 30 na endapo itashindikana, basi watachukua uamuzi wa kumuua.

Kwa miaka kadhaa ya hivi karibuni, maeneo mengi ya Nigeria, hasa Kaskazini, yamekuwa yakikabiliwa na matukio ya utekaji.

Matukio hayo yameshuhudiwa kwa wingi zaidi katika majimbo ya Zamfara, Katsina, Kaduna, Sokoto, Niger na Kogi.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...