MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI SABA YA BILIONI 51.825 ILALA

Date:

Share post:

MWENGE wa Uhuru umepokelewa jijini Dar es Salaam Aprili 13, 2026 na kuanza mbio zake katika Wilaya ya Ilala, ukitarajiwa kupita katika maeneo mbalimbali huku ukizindua na kukagua miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 51

Mwenge huo umepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ukitokea Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar. Baadaye ukakabidhiwa rasmi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

Akipokea Mwenge huo, Mpogolo amesema katika wilaya hiyo Mwenge utakimbizwa kwa takribani kilomita 54, ukikagua na kuzindua miradi hiyo ya maendeleo, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Mwenge huo umezindua Mradi wa Kitega Uchumi eneo la Kariakoo, hatua inayotarajiwa kuongeza fursa za kipato na kukuza biashara ndogondogo.

Aidha, katika sekta ya miundombinu, Mwenge umekagua ujenzi wa Barabara ya Lindi kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 1.015, mradi unaolenga kuboresha usafiri na kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

Mwenge wa Uhuru pia unazindua miradi mbalimbali ikiwemo kisima cha maji na kituo cha afya katika eneo la Mchikichini, hatua inayotarajiwa kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...