PWANI WAANZA KUKAGUA MIRADI YA MWENGE WA UHURU 2026

Date:

Share post:

Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Pwani imeanza rasmi ukaguzi wa miradi inayotarajiwa kuzinduliwa na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mapokezi ya mbio hizo muhimu kitaifa.

Ukaguzi huo ulioanza Aprili 10, 2026, unahusisha miradi mbalimbali katika halmashauri zote za Mkoa wa Pwani. Lengo kuu ni kuhakikisha miradi yote ipo katika hali nzuri na iko tayari kwa ajili ya uzinduzi wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru.

Kwa mujibu wa ratiba, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili mkoani Pwani Aprili 18, 2026, ukitokea Mkoa wa Dar es Salaam. Utapokelewa rasmi katika Wilaya ya Bagamoyo, ambako utakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma kwa wananchi.

Aidha, Aprili 27, 2026, Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa Mkoa wa Lindi baada ya kukamilisha ziara yake katika Mkoa wa Pwani.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...