NINI CHANZO ‘UADUI’ WA AFRIKA KUSINI, MAREKANI?

Date:

Share post:

LOS ANGELES, Marekani

HIVI karibuni, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alitoa kauli tata aliposema kwa sasa dunia inaendeshwa kidikteta.

Kwa wafuatiliaji wa siasa za kimataifa, kauli hiyo ilimlenga moja kwa moja Donald Trump, ambaye utawala wake umeivamia Venezuela na kisha kuishambulia Iran.

Kwa muda sasa, uhusiano wa Afrika Kusini na Marekani umedorora na ni tangu Rais Trump aliporejea madarakani mwaka 2025.

Trump amekuwa hafichi hisia zake, kwamba Serikali ya Afrika Kusini imekuwa ikipuuza haki za watu weupe nchini humo.

Kwa madai yake, ambayo hata hivyo yanakosa ushahidi, watu wenye ngozi nyeupe wamekuwa wakiteswa na hata kuuawa, huku Serikali ikiwa kimya tu.

Kuonesha hasira zake, aligomea kushiriki Mkutano wa G20 wa mwaka 2025 uliofanyika katika ardhi ya Afrika Kusini.

Zipo taarifa kuwa Marekani sasa inajaribu kushawishi Afrika Kusini inyimwe nafasi ya kushiriki Mkutano wa G7 utakaofanyika Juni, 2026 huko Ufaransa.

Lakini, kwa mujibu wa mchambuzi wa siasa wa Afrika Kusini, Daniel Silke, uhusiano mbaya kati ya Taifa hilo na Marekani ulianza miaka 10 iliyopita, yaani kabla ya Rais Trump kurudi Ikulu.

“Miaka 10 iliyopita, Afrika Kusini ilibadili mwelekeo wa sera zake za nje kwa kuzipa kisogo Marekani na mataifa ya Magharibi,” anasema Silke.

Kwamba Afrika Kusini iliamua kujiingiza BRICS, ambao ni umoja wa nchi zinazokuja juu kiuchumi, baadhi ya wanachama wake wakiwa ni Urusi na China.

“Marekani imekuwa ikifuatilia ajenda za BRICS, ambayo lengo lake kubwa ni kuua nguvu ya dola katika soko la dunia,” anasema.

Kwa upande wake, Dianne Hawker, anasema Trump alikuwa akiipigia hesabu Afrika Kusini hata kabla ya kurudi Marekani.

“Wiki mbili tu baada ya kuapishwa, Trump alitangaza kuwa Marekani imesitisha misaada yake yote kwa Afrika Kusini kwa madai kuwa imekuwa ikikiuka haki za binadamu,” anasema Hawker.

Aidha, wapo wanaoamini kuwa ni ngumu kiasi fulani kuzitenganisha Afrika Kusini na Urusi, ambazo uhusiano wake unatajwa kuwapo tangu miaka ya 1970.

Wakati ambao Urusi iliiunga mkono Afrika Kusini iliyokuwa ikipambana kujinasua katika minyororo ya wakoloni (Waholanzi).

Afrika Kusini haijasahu kuwa Marekani chini ya Rais  Ronald Reagan ingeweza kuingilia kati na kuisaidia kupambana na wakoloni lakini haikujishughulisha.

Hata katika mgogoro unaoendelea kati ya Marekani na Iran, Afrika Kusini imejipambua kuwa iko upande wa Taifa hilo la Kiarabu.

Si tu kwa sababu haina uhusiano mzuri na Marekani, bali pia kuna urafiki wa miaka mingi uliopo kati ya Afrika Kusini na Iran.

Wakati wa mapambano ya kuondosha ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, Iran iliwachukulia hatua wakoloni (Waholanzi) kwa kuwanyima huduma ya mafuta.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...