SHABIKI KUISHITAKI ARSENAL KWA KUMSABABISHIA ‘STRESS’

Date:

Share post:

KAMPALA, Uganda

SHABIKI wa Arsenal raia wa Uganda, Eric Kyama, anajiandaa kuifungulia mashitaka klabu hiyo kwa kile alichodai imemsababishia changamoto za kisaikolojia, hasa huzuni na msongo wa mawazo.

Mkazi huyo wa Kampala, amesema hatua yake hiyo imetokana na kuumizwa zaidi na matokeo ya mchezo uliopita dhidi ya Bournemouth.

Arsenal iliyoko kileleni mwa msimamo wa Ligi, ilishindwa kuongeza pengo la pointi kati yake na Manchester City baada ya kufungwa mabao 2-1.

Kwa matokeo hayo, sasa Arsenal inaongoza Ligi kwa pointi sita pekee, baada ya Man City kuifunga Chelsea mabao 2-1.
“Naandika taarifa hii rasmi juu ya nia yangu ya kufungua mashitaka dhidi ya klabu ya soka ya Arsenal, wachezaji na kocha Mikel Arteta kutokana na kiwango walichokionesha dhidi ya AFC Bournemouth.”imeeleza taarifa yake.

Shabiki huyo amesema katika mashitaka yake, anailalamikia Arsenal si tu kwa kupuuza weledi na ushindani ndani ya uwanja, bali pia kutokujali hisia za mashabiki wake.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

XI JINPING AKUTANA NA SHEIKH MOHAMMED BIN ZAYED KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHINA NA UAE

Beijing, China Rais wa China, Xi Jinping, amekutana na Mwenyekiti wa Abu Dhabi na Rais wa Falme za Kiarabu...

RAIS MWINYI AKAGUA MRADI WA MJI WA AFCON

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea na kukagua maendeleo ya...

TRUMP AFUTA PICHA YAKE AKIJIFANANISHA NA YESU AKIDAI IMETAFSIRIWA VIBAYA

Washington, Marekani Rais wa zamani wa Marekani, Donald J. Trump, ametoa ufafanuzi kufuatia picha aliyochapisha katika mtandao wake wa...

CHELSEA WAMTUPIA JICHO WILLIAM GOMES

London, Uingereza Klabu ya Chelsea imeendelea kuonyesha nia ya dhati ya kumsajili kiungo wa pembeni wa FC Porto, William...