MAHAKAMA TATU ZA MWANZO ZAZINDULIWA JIJINI ARUSHA

Date:

Share post:

AJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, Frank Habibu Mahimbali, amezindua majengo matatu ya Mahakama za Mwanzo na kurasimisha kuanza kwa shughuli za utoaji haki katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha.

Mahakama hizo zimejengwa katika wilaya za Longido (Kata ya Kitumbeine), Arusha (Kata ya Terati) na Monduli, huku hafla ya uzinduzi ikifanyika katika Mahakama ya Mwanzo ya Makuyuni, wilayani Monduli.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Jaji Mahimbali amesema hatua hiyo ni matokeo ya dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati na kwa gharama nafuu bila ubaguzi.

“Ufunguzi wa mahakama hizi ni utekelezaji wa azma ya serikali ya kusogeza huduma za haki karibu zaidi na wananchi,” amesema Jaji Mahimbali.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Monduli, . Gloriana Kimath,amesisitiza umuhimu wa watumishi wa mahakama kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...