KAMATI ZA BUNGE KUANZA VIKAO LEO DODOMA

Date:

Share post:

 

Spika wa Bunge, Job Ndugai

NA MWANDISHI WETU

KAMATI  za kudumu za Bunge zinaanza vikao vyake leo jijini Dodoma kutekeleza majukumu ya kibunge kabla ya kuanza kwa mkutano wa pili wa Bunge la 12, Februari 2, 2021.

Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za kamati iliyotolewa wiki iliyopita na kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa cha Bunge, shughuli ya kwanza itakayofanywa na kamati zote ni kuchagua wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati.

Baada ya kupatikana kwa viongozi wa kamati, wabunge wataanza kupewa mafunzo kuhusu taratibu za uendeshaji wa kila kamati ambayo yatafuatiwa na mafunzo kuhusu Bunge mtandao na usalama wa mtandao kwa kamati zote.

Ratiba inaonyesha kuwa shughuli nyingine itakayofanyika ni kamati za kisekta kupokea maelezo ya wizara kuhusu muundo, majukumu ya taasisi, sera na sheria zinazosimamiwa na wizara hizo.

“Mafunzo kwa Kamati za Hesabu za Serikali (PAC) Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) na Kamati ya Bajeti kuhusu uchambuzi wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Msajili wa Hazina (TR)  na namna bora ya kuhoji maafisa masuhuli.

“Mafunzo kwa kamati ya sheria ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo na uzoefu wa mabunge mengine ya nchi zinazofuata mfumo wa kibunge wa Jumuiya ya Madola,” inasomeka ratiba hiyo.

Kuhusu shughuli zitakazofanywa na kamati ya bajeti, ratiba hiyo inaonyesha kamari ya bajeti itapokea na kujadili taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa mpango wa pili wa maendeleo ya taifa kwa miaka mitano 2016/17 – 2020/21.

Inaonyesha zaidi kuwa kamati hiyo itapokea na kujadili mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano 2021/22-2025/26 na mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya taifa wa mwaka mmoja 2021/21.

Shughuli nyingine zilizomo kwenye ratiba hiyo ni kamati ya bajeti kupokea na kujadili mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya serikali pamoja na sheria ya fedha kwa kipindi cha nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MAREKANI, CUBA: MZOZO MWINGINE UNAOSUBIRI KUITIKISA DUNIA

HAVANA, CubaRAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, hajaonesha unyonge, licha ya Taifa lake kuendelea kupewa presha kubwa na Rais...

LINDI YAIMARISHA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA WASH KUBORESHA AFYA ZA WANANCHI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary, amesema mkoa huo unaendelea kunufaika na utekelezaji wa afua...

WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA KWA ZIARA YAKE YA KIKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewasili mkoani Arusha kwa ziara...

BARAZA LA MADIWANI MTAMA LAKUTANA, LAPONGEZA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAENDELEO

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama limefanya kikao chake cha robo ya tatu kwa mwaka...