RAIS DK. MAGUFUILI AFARIKI DUNIA

Date:

Share post:

 

Hayati Rais  Dk. John Magufuli

NA CHARLES MULLINDA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniam, Dk. John Pombe Magufuli amefariki dunia katika Hospitali ya Mzena, iliyopo jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelitangazia taifa, leo Machi 17, 2021 majira ya saa tano usiku kuwa Rais Dk. Magufuli amefariki kutokana na maradhi ya moyo.

Akizungumza na Taifa kutokea mkoani Tanga, Makamu wa Rais Samia amesema Rais Dk. Magufuli amefariki dunia majira ya saa 12 jioni baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Machi 14, mwaka huu.

Makamu wa Rais Samia amesema awali Rais Dk. Magufuli alifikishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Machi 6, mwaka huu akisumbuliwa na tatizo la moyo la mfumo wa umeme ambalo amekuwa nalo kwa zaidi ya miaka 10.

“Machi 14 mwaka huu, alijisikia vibaya akakimbizwa Hospitali ya Mzena ambako aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete hadi umauti ulipomkuta,” amesema Makamu wa Rais Samia.

Amesema Tanzania itakuwa katika kipindi cha maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti.

Aidha Makamu wa Rais Samia, amesema wananchi watajulishwa juu ya taratibu za mazishi za Rais Dk. Magufuli.


 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...