ZITTO KWABWE AOMBOLEZA KIFO CHA RAIS DK. MAGUFULI

Date:

Share post:

 

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe

NA CHARLES MULLINDA

KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema amepokea kwa masikitiko na huzuni habari za kifo cha Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dk. John  Magufuli kilichotangazwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Machi 17, majira ya saa tano usiku akiwa mkoani Tanga.

Zitto ameeleza hayo katika tamko lake rasmi na lenye saini yake linaloeleza zaidi kuwa Hayati Rais Dk. Magufuli wakati wa uhai wake amekuwa kiongozi wa nchi katika nyadhifa mbalimbali  na kwa hakika alitekeleza wajibu wake kwa juhudi kubwa na kwamba taifa litamkumbika kwa mchango wake kwenye maendeleo ya nchi.

“Kwa niaba ya Chama cha ACT Wazalendo na kwa niaba yangu binafsi natoa pole kwa mama yetu Janeth Magufuli na familia nzima ya hayati John Pombe Magufuli, tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu. Natuma salamu zangu za rambirambi kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na wanachama wa CCM kwa kuondokewa na mwenyekiti wao wa taifa.

“Natoa pole kwa Rais Mteule, ndugu Samia Hassan kwa msiba huu mzito kwa taifa letu. Katika nyakati hizi za majonzi makubwa tunamtakia rais mteule kheri, ujasiri na ushupavu katika kutekeleza majukumu yake,” inasomeka sehemu ya taarifa ya Zitto.

Aidha, Zitto anaandika kuwapa pole watanzania wote kwa msiba mkubwa na kuwaombea wawe na moyo wa subira, mshikamano na umoja katika kipindi kigumu cha maombelezo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...