WANAFUNZI SEKONDARI BULYAGA WAASWA KUKABILIANA NA UKATILI

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA

MTANDAO wa Polisi Wanawake (TPF NeT) Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya umewataka Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bulyaga kushiriki kutokomeza ukatili katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na Mkaguzi wa Polisi, Fausta Ndumbaro walipotembelea shule hiyo Machi 04, 2026 na kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Mkaguzi wa Polisi Ndumbaro amewataka wanafunzi hao kushirikiana na Jeshi la Polisi na taasisi nyingine katika vita ya kuzuia na kutokomeza vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto kwa kutoa taarifa na kuwafichua wanaofanya vitendo hivyo.

Naye, Polisi Kata ya Kinyala, Mkaguzi wa Polisi, Lusajo Kibonde amewakumbusha wanafunzi hao wajibu wao kama watoto katika familia ikiwemo utoaji wa taarifa za viashiria vya uhalifu, kusaidia wazazi/walezi kazi za nyumbani na kusoma kwa bidii.

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lipo katika muendelezo wa utoaji elimu ya kijinsia na ukatili kwa makundi mbalimbali ya kijamii ili kuyajengea uwezo na uelewa wa masuala hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...