KISHINDO CHA IDAHAMS KWENYE ‘MAN ON FIRE’ NI BALAA

Date:

Share post:

Idahams


MWANDISHI WA PANORAMA

MSANII anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Nigeria, Idahams amefanikiwa kukivuka kikwazo cha maradhi ya covid 19 kwa kuachia albamu maalum (extended play- ep) iitwayo ‘man on fire’ yenye jumla ya nyimbo saba zilizobeba ujumbe wa kuwafariji na kuwapa moyo watu wote katika kipindi hiki kigumu ambacho dunia inapambana na janga la corona.

Nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo ni mchanganyiko wa aina mbalimbali za muziki ikiwemo afro pop, rap na aina nyingine hususan unaopatikana barani afrika, ukiwemo wimbo wa ada na man on fire alizoshirikiana na mwanamuziki Falz, Shima alioshirikiana na Peruzzi na Seyi Shay.

Katika albamu hiyo, Idahams anaendeleza moto aliouwasha mwaka 2020 kwa kutoa nyimbo kali zaidi ya zile zilizopo kwenye albamu yake iliyopita kama belle, god when na no one else alioutoa mwaka 2018 ambao ulisababisha asainiwe na lebo kubwa za Universal Music na Grafton Records.

Katika albamu hiyo, Idaham ameendelea kuonesha uwezo mkubwa wa namna anavyoweza kutunga nyimbo zenye mashairi mazito, zilizoandaliwa na maprodyuza bora kwa kuzingatia asili yake ya kusini mwa Nigeria sambamba na midundo mizuri inayomfanya kuendelea kuwa msanii tishio barani afrika.

 

 

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...