Sunday, June 15, 2025
spot_img

WASANII, WANAMUZIKI WAITWA RUMANYIKA – KARAGWE KUREKODI ‘MOVIE’, MUZIKI

RIPOTA PANORAMA

WASANII wa filamu na wanamuziki wa hapa nchini na Afrika kwa ujumla wamealikwa Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika – Karagwe kwenda kurekodi kazi zao kwa kuchangia gharama kidogo.

Mwaliko huo umetolewa hivi karibuni na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, ambaye pia ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika – Karagwe, Charles Ngendo alipofanya mahojiano na Tanzania PANORAMA Blog kuzungumzia pamoja na mambo mengine, upekee wa vivutio vya hifadhi hiyo.

Ngendo alisema mandhari nzuri, hali ya hewa, wanyama wa aina mbalimbali, ndege wa majini na nchi kavu, milima na mabonde vilivyopo kwenye Hifadhi ya Rumanyika – Karagwe vinafaa kupamba kazi za wasanii wa filamu na wanamuziki.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika – Karagwe, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Charles Ngendo

“Naomba kutumia jukwaa lako Tanzania PANORAMA Blog kuwaalika wasanii wa filamu na wanamuziki wa hapa nchini na Afrika yote, waje wafanye kazi zao kwenye Hifadhi ya Rumanyika – Karagwe.

“Najua watu watauliza gharama, niwambie, wakati mwingine hifadhi zetu zimekaa kikutoa huduma zaidi, bei ni sawa na bure. Kwa sasa tunatoza Shlingi 100,000 kwa kundi la watu kuanzia wawili hadi 20 wanaorekodi video kwa ajili ya matumizi binafsi iwe muziki au maigizo.

“Hifadhi hii ina wanyama wa kila aina, milima yenye misitu ya Kiikweta, Bonde la Kishanda lenye maziwa na mandhari ya kuvutia ambayo mwimbaji akirekodi filamu ya wimbo wake hapo, duniani nzima itatamani kuuangalia kwa sababu tu ya mandhari ya eneo hilo.

Msanii wa filamu, Irene Uwoya

“Nizungumzie gharama kidogo, ndani ya hifadhi kurekodi video za muziki au filamu ni Shilingi 100,000 kwa siku na kwenye viwanja vya Ofisi za Makao Makuu, gharama ni hiyo hiyo kwa watu 50,” alisema Ngendo.

Alisema, wasanii wanaweza pia kula chakula porini kama watalii wengine kwa gharama ya Shilingi 5,000 na wanaweza kufanya utalii wa boti kwa kulipa Shilingi 10,000.

Akizungumzia tozo zilizowekwa kwa makundi ya wanafunzi wanaotembelea hifadhi hiyo, Ngendo alisema tozo ya uhifadhi kwa shule za msingi, sekondari na kidato cha tano na sita ni Shilingi 2,000 tu na kwa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu ni Shilingi 5,000.

Mbweha anayepatikana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika – Karwagwe

Alisema tozo ya kupiga kambi kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na kidato cha tano na sita ni Shilingi 2,000 na wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu ni Shilingi 3,000 huku malazi kwa nyumba na hosteli kwa wanafunzi ni Shilingi 5,000.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya