Tuesday, December 24, 2024
spot_img

BITEKO AZINDUA TAARIFA ZA UTENDAJI KATIKA SEKTA YA NISHATI

*Ataka changamoto zilizoainishwa zipatiwe majibu ndani ya miezi mitatu
*Aelekeza EWURA kupima uhusiano wa rasilimali na mabadiliko ya maisha ya watu
*Asema wizara, taasisi zitoe kipaumbele kwa Sekta Binafsi

*Uwekezaji gesi asilia, mafuta na umeme waongezeka
*JNHPP yaingiza mtambo wa pili katika gridi ya Ta
ifa

TERESIA MHAGAMA

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amezindua taarifa za utendaji katika sekta ndogo ya umeme, gesi asilia na mafuta kwa mwaka 2022/2023.

Akizindua; ametoa maelekezo mahsusi kwa wizara na taasisi mbalimbali kufanyia kazi taarifa zinazoonesha mafanikio na changamoto katika Sekta Nishati.

Dk. Biteko alizindua taarifa hizo Juni 14, 2024 Jijini Dodoma, kwa kuagiza taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Wizara ya Mipango na Uwekezaji kusoma taarifa hizo na kuzichambua na changamoto zilizoainishwa zipatiwe majibu ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Aidha, ameagiza fursa zote zilizoonekana kwenye taarifa hizo zichukuliwe kwa uzito mkubwa na ufanyike utambuzi wa watu wenye uwezo wa kuzitumia kwa watumishi walioko serikalini na taasisi binafsi.

“Vilevile nawaagiza EWURA mhakikishe kuwa, tathmini ya mwaka ujao ihusishe utendaji wa Nishati Safi ya kupikia ili kuweza kujipima kwa usahihi kuhusu utekelezaji wa ajenda hii inayopewa kipaumbele na Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Dk. Biteko

Agizo jingine alilolitoa lilihusu vitisho  vilivyoainishwa kunyemelea Sekta ya Nishati
katika ripoti ya mwaka 2023 hadi 2025  viwekewe mabunio ya suluhisho lake ili katika ripoti ijayo, changamoto husika zisiwepo ikiwemo suala la kuongezeka kwa mahitaji ya umeme kila mwaka.

Dk. Biteko pia ameitaka EWURA kupima uhusiano wa rasilimali zilizopo na mafanikio ya watu ambapo amesisitiza kuwa mafanikio ya sekta lazima yaendane na mabadiliko ya maisha ya watu.

Pia ametaka mifumo ya uagizaji mafuta iendelee kuboreshwa baada ya kufanyika utafiti wa kina na kueleza kwamba miundombinu ya mafuta bado inahitajika huku akisisitiza kuwa urasimu usiwepo kwenye Sekta ya Nishati.

Ameipongeza  EWURA kwa tathmini ambayo inaonesha kuwa Sekta ya Nishati inaendelea kuimarika, akitolea mfano kutolewa kwa leseni ya kuchimba gesi asilia katika kisima cha Ntorya kilichopo mkoani Mtwara kitakachotoa gesi futi za ujazo milioni 140 kwa siku ambapo leseni ya mwisho ya kuchimba gesi ilitolewa mwaka 2006.

Kuhusu sekta ndogo ya umeme amesema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuiboresha ambapo leo ametoa taarifa kuwa mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) umeingiza mtambo wa pili katika gridi ya Taifa kupitia mtambo namba 8 na hivyo kufanya mradi huo kuingiza megawati 470 katika gridi.

Kuhusu sekta binafsi amesema, “Sekta binafsi imetutoa kimasomaso, serikali haiwezi kufanya kila kitu, wamefanya kazi kubwa mno kwenye mafuta, gesi na hata kwenye uzalishaji umeme, wito wangu kwenu msibaki nyuma, changamkieni fursa na kwa taasisi zilizo chini ya wizara msione sekta binafsi kama watu wajanja wajanja, tuwape ipaumbele,” alisema Dk. Biteko

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule,
amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiimarisha Sekta ya Nishati na kusema kuwa Dodoma imeshuhudia matunda ya uimarishaji huo wa sekta kwani sasa umeme haukatiki.

Pia amepongeza utashi mkubwa wa uongozi wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ambao unachangia kwa kiasi kikubwa kuiimarisha sekta kwa ujumla.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa katika tathimini iliyozinduliwa inaonesha sekta imepiga hatua kwenye maeneo megi ikiwemo uhakika wa upatikanaji umeme, upatikanaji na usambazaji wa mafuta kuimarika hasa baada ya Dk. Doto Biteko kuanza kuongoza Wizara ya Nishati./

Aidha, alisema upatikanaji na uwekezaji wa gesi unaendelea kuimarika ikijumuisha usambazaji gesi kwenye maeneo mbalimbal .kama magari, majumbani na viwandani.

Alisema taarifa ya Benki ya Dunia kwa Nchi za Dunia ya Tatu zinazofadhiliwa na benki hiyo inaonesha kuwa Sekta ya Nishati kwa
Tanzania inafanya vizuri zaidi kati ya Nchi zote zinazoendelea na Bara la Afrika kwa ujumla.

Mramba alisema hayo ni matunda ya usimamizi madhubuti wa Dk. Biteko ambapo  eneo lililofanya vizuri zaidi ni usambazaji umeme vijijini na miradi mingine ya nishati kama JNHPP na mradi wa TAZA.

Alisema Benki ya Dunia imeidhinisha Dola.za Marekani milioni 300 ili ziendeleze sekta ya umeme kutokana na ufanisi huo wa Tanzania.

Akitoa taarifa za utendaji katika Sekta ya Nishati, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile alisema kuwa Sekta ya Nishati inaendelea kuimarika ikiwemo uwekezaji kwenye miundombinu ya mafuta, uwekezaji wa vituo vya mafuta.

Alisema kuna ongezeko la uagizaji wa gesi ya mitungi (LPG) kwa asilimia 16 na ongezeko la uagizaji wa mafuta kwa asilimia 8.

Andilile alisema kwenye sekta ya umeme, uwekezaji umeongezeka katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji na kwamba upotevu wa umeme unazidi kupungua na wateja wa umeme wameongezeka kutoka milioni 3.8 mwaka 2021/22 hadi milioni 4.4 mwaka 2022/2023.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya