Wednesday, June 25, 2025
spot_img

MUME ANAYELIA KUTESWA NA MKEWE, KUTELEKEZWA NA WATOTO (1)

 

Laiser Marko na Mkewe Pamela Kayira siku ya siku harusi yao

*Ni Laizer Marko anayehofia usalama wa maisha yake ndani ya ndoa, bosi Mamlaka ya Chakula na Lishe aficha siri

*Aomba huruma ya mkware anayevuruga familia yake, azungumzia uraia wa mkewe na shemeji yake

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

TUHUMA za usaliti wa mapenzi zimeibua hofu na wasiwasi katika familia ya wanandoa wawili, Laizer Marko na Pamela Kayira, wakazi wa Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.

Laizer Marko, mume wa Pamela Kayira ndiye anayefichua kuwepo kwa hali ya hofu na wasiwasi ndani familia yake katika mahojiano aliyoyafanya na Tanzania PANORAMA Blog hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine anamtuhumu mkewe kuwa chanzo cha kuwepo kwa hali hiyo kwa kuisaliti ndoa yao.

Katika mahojiano hayo, Marko anamtuhumu Pamela kuwa na uhusiano wa mapenzi na mwanamume mwingine, kuitelekeza familia yake, (mumewe Maiko na watoto wao watatu), kuwa na kiburi na jeuri, kuondoka nyumbani asubuhi kwenda kazini na kurudi asubuhi ya siku inayofuata akiwa hajulikana alikolala huku akijua kuwa uraia wake pamoja na wa dada yake ni wa mashaka pamoja  na kuhama nyumbani kwake kwa muda wa miezi sita kwenda kuishi mahali kusikojulikana.

Marko anasema amemgundua mkware mwenye uhusiano na mkewe na anamuomba amuonee huruma kwa sababu kitendo anachokifanya kina athari mbaya katika maisha ya watoto wake na kinaiharibu familia yake. Pia anamuomba mwajiri wa mkewe asaidie kuokoa ndoa yake na watoto kupata mapenzi na malezi ya mama yao.

Kwa upande wake Pamela anazipuuza tuhuma hizo. Katika mahojiano aliyofanya na Tanzania PANORAMA Blog, Pamela anakataa kutoa ushirikiano na anaikana ofisi anayofanyia kazi.

Wakati Pamela anapuuza tuhuma na kilio cha mumewe, bosi wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Germana Leyna naye anakataa kuthibitisha kama Pamela ni mfanyakazi wa taasisi anayoiongoza au lah na anajiweka mbali na ombi la Maiko la kumkalisha kitako Pamela ili kumsihi kuijali familia yake na hasa kulea watoto wake.

Tanzania PANORANA Blog ambayo imefuatilia mkasa huu kwa kina imeandaa makala maalumu ikianza na mahoajino iliyoyafanya na Marko anayeeleza kinaga ubaga historia ya maisha baina yake na mkewe, mateso anayoyapata ndani ya ndoa, hofu aliyonayo kuhusu maisha yake na watoto na wasiwasi wa nyendo na uraia wa mkewe  pamoja na dada yake. Kwa maneno yake mwenyewe, analeeza.    

“Ni kweli kwamba Pamela ni mke wangu. Tulifunga ndoa miaka 17 iliyopita, mwaka 2005, Aprili 2, tuliishi kama wachumba miaka mitatu nyuma kwa hiyo jumla tuna miaka kama 20.

Laizer Marko na Mkewe Pamela


 

“Ni kweli kwamba nina watoto naye na ni kweli kwamba mara kwa mara huwa anawatelekeza anaenda kusikojulikana na kwa uchunguzi tu ambao nilioufutilia na nimekwishashika meseji zake za mapenzi.

“Nilishika meseji za simu za mapenzi, mawasiliano ya kipenzi kwenye meseji za simu na nilizigundua tarehe 28, Januari mwaka huu. Niliripoti lakini yeye akatumia nafasi hiyo kwenda kushtaki kuwa nimempiga na vitu kama hivyo.

“Kuna mtu mmoja mwanamume anaitwa (anaitaja jina) ambaye katika hizo meseji ni kwamba ni mfanyakazi anayefanya kazi hospitali ya (anaitaja jina) iliyoko Oysterbay karibu na Kanisa la St. Peter’s.

“Sijawahi kubaini mwenendo wake mwingine zaidi ya huo, isipokuwa mwenendo wake mbaya tu. Tetesi mbalimbali nilizokuwa nikiambiwa kuwa huyu ni lazima atakuwa na mtu nilikuwa nikidhani kuwa ni mambo ya kusikia tu lakini ndiyo nilikuja kushuhudia kabisa.

“Tulikaa kikao cha nyumbani ambacho na yeye alihusika, ilikuwa tarehe 14, Februari mwaka huu, kwa upande wa wazazi, wa kwangu na wa kwa upande wake yeye kwa hiyo katika kuongea nikawaambia basi huyu nitaendelea kumfuatilia, wakaniambia hapana, nisimfutilie, akiwemo dada yake na yeye.

“Walianiambia nisimfutulie kwa hiyo sijawahi kuwasiliana naye kabisa. Huyu ni mke wangu wa ndoa na tulioana kanisani na cheti cha ndoa tunacho. Tulifunga ndoa katika Kanisa la Azania Front.

“Ni mjeuri sana, anajibu hovyo. Haheshimu kiapo cha mchungaji wala nini. Juzi tu hapa, jumatani iliyopita amelala nje, juzi tu hapa alipoenda kazini hakurudi nyumbani. Yaani yeye anajiamulia muda wowote anafanya anavyojua.

“Mimi tangu alipoanza hizi jeuri na tulipokaa kikao cha wazazi tarehe 18, Februari mwaka huu aliondoka nyumbani kama miezi sita akawa hajulikani anakaa wapi.

“Alikuwa anakuja kuchungulia watoto anaondoka. Nikawa nimeripoti kwa wazazi kuwa huyu aliambiwa aje na kikao rasmi cha wazazi lakini anakuja anachungulia watoto anaondoka, saa nyingine anakuja analala kwa watoto sasa likitokea jambo lolote baya watasema yupo kwa nani?

“Wakasema. Upande wa wazazi nitulie tu nimwangalie mpaka mwisho kwa sababu pengine kuna kitu anatafuta ili pengine labda akakushtaki. Kwa hiyo kuanzia hapo nikawa nimetulia tu.”

ITAENDELEA

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya