Wednesday, June 25, 2025
spot_img

MSTAAFU ATAPELIWA MAMILONI YA MAFAO

Dula la mitungi ya gezi la minaz


RIPOTA PANIRAMA

0711 46 49 84

ROMANUS SHIRIMA, ambaye alistaafu kazi na kulipwa mafao yake, ametaperiwa na mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia anayedai alimlaghai kuingia naye ubia wa kufanya biashara ya kuuza mitungi gesi.

Akizungumza na Tanzzania PANORAMA Blog nyumbani kwake Mbezi Msigani, Kinondoni, hivi karibuni, Shirima alimtaja mtu aliyempateri kwa jina la Minaz

Alisema mara tu baada ya kustaafu na kulipwa mafao yake Minaz ambaye anafanya biashara ya kuuza mitungi gesi, alimfuata na kumshawishi aingize pesa zake za mafao kwenye biashara yake huku akimuahudi kuwa watakuwa wanagawana  faida. 

Shirima ambaye kwa sasa alidai kuwa na matatizo ya afya yake alisema alimuamini Minaz baada ya kumuona ni muhindi hivyo akampatia pesa zake zote za mafao ili aziingize kwenye biiashara yake.

Alisema baada ya kumpatia fedha hizo, Minaz alianza kumkwepa na hakuonana naye kwa zaidi ya mwaka mmoja na kipindi hicho chote hakumpa mgawo waliokubaliana hivyo akalazimika kuanza kuishi maisha ya kuombaomba.

“Hii dunia hufaja hujaumbika. Dunia imenigeuka. Huyu muhindi kanifanyia kitu kibaya sana, alikuja kwangu vizuri akanishawishi nimpe pesa zangu za mafao aziingize kwenye biashara yake ya mitungi ya gesi na mimi nitakuww mbia wake lakini nilipompa pesa yangu kanikimbikia.

“Pesa yote kachukua, hapa ninaumwa sina uwezo wa kupata matibabu kwani sina pesa. Wanangu nimeshindwa kuwapia ada ya shule, maisha yangu yameharibika. Nilipompa pesa akaanza kunikimbia zaidi ya mwaka hajanipa chochote tofauti na makubaliano yetu.

“Baadaye ndiyo mara moja moja akawa ananipa mara laki moja mara elfu hamsini nazo kwa shida. Kila nikimfuata anasingizia ugonjwa, mara aseme ana betri moyoni, mara kisukari kila aina ya ugonjwa anajipa yeye wakati mzima kabisa. 

“Najua nitakufa na atabaki na hela zangu zaidi ya milioni 12 nilizompa. Mungu atamlipia lakini la muhimu ninalotaka kusema ni kwamba wastaafu tuwe nakini sana tunapolipwa mafao yetu, kuna watu wengi wanatunyemelea na wanakuja kwa sura ambazo wala huwezi kujua kuwa ni watu wabaya kumbe ndiyo mbwa mtu,” alisema.

Alipotafutwa Minaz na kuulizwa kuhusu malalamiko hayo alisema ni kweli anadaiwa na Shirima lakini anamlipa kidogo kidogo kutokana na hali ya biashara ilivyo.

Alksena kwa sasa anaumwa ugonjwa mkubwa na yupo nje ya nchi kwa matibabu ila atakaporudi ataendelea kumlipa.

“Mimi sikatai kuwa ananidai lakini kwani deni linamfunga mtu? Alinipa pesa ndiyo kwa sababu tufanye biashara lakini biashara siyo nzuri hivyo namlipa kidogo kidogo kila ninapopata.

“Kwa sasa siwezi kumlipa kwani niko nje ya nchi kwa matibabu ambayo yatachukua zaidi ya mwezi mmoja na nusu tuombe Mungu matibabu yangu yakienda vizuri nitarudi nchini nitaendelea kumlipa,” alisema Minaz.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya