KILA KONA TANZANIA KUFIKISHIWA UMEME

Date:

Share post:

TERESIA MHAGAMA

Dodoma

SERIKALI inaendelea kutekelezaji kazi ya kusambaza miundombinu ya Nishati ya Umeme katika kila kona ya eneo la nchi.

Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa jana, bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Masasi, Geofrey Mwambe.

Katika swali lake, Mwambe aliihoji Serikali kuwa ni itapeleka umeme kwenye Vijiji vya Namikunda, Chipole, Machombe, Mtakateni, Machenje, Matawale, Mpekeso, Chakama na Kata ya Temeke.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Kapinga alisema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), inatekeleza mradi wa kusambaza umeme vijijini wa awamu ya tatu, mzunguko wa pili ambapo vijiji vyote visivyokuwa na umeme Tanzania bara vitafikishiwa.

 Naibu Waziri Kapinga alisema kazi ya kusambaza miundombinu ya umeme katika vijiji 17 vya Jimbo la Masasi inafanywa na Mkandarasi NAMIS Corporate Limited.

Alisema hadi Agosti 15, mwaka huu NAMIS Corporate Limited imekwishasambaza miundombinu hiyo kwenye vijiji 11 na vijiji sita zilivyosalia, kazi itakamilika kabla ya mkataba wa mkandarasi kuisha Disemba 31, 2023.

Aidha, Naibu Waziri Kapinga alisema Vijiji vya Namikunda, Mtakateni, Matawale, Mpekeso na Chakama tayari vina umeme.

Naibu waziri huyo alisema hivi sasa kazi ya kusimamisha nguzo katika Kata ya Temeke (Mkarango) inaendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...