MAJALIWA ATAKA VIJANA WAENDELEZWE

Date:

Share post:

RIPOTA WA WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi na wataalamu wa mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka nguvu zaidi katika kuwaendeleza vijana ili washiriki kikamilifu shughuli za kiuchumi na kuwapata ujuzi na mbinu za ujasiriamali.

Majaliwa alitoa agizo hilo Agosti 8, mwaka huu alipokuwa akifunga kongamano la vijana lililofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.

Alisema vijana wanapaswa kupatiwa  mbinu na ujuzi wa ujasiriamali ili waweze kuchangamkia fursa zilizo mbele yao.

Aliagiza kila mkoa kuandaa mpango mahsusi wa kuhamasisha vijana kufanya shughuli zenye staha na kuwavutia vijana wengi kushiriki shughuli za kiuchumi. 

Majaliwa alizitaka taasisi na mifuko ya uwezeshaji kwa vijana zitangaze fursa zilizopo na zitumie mbinu mbalimbali zikiwemo redio za kijamii kuwafikia walengwa.

“Kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki kuwapa taarifa, kuwaongoza na kuwaunganisha vijana na fursa mbalimbali za kukuza mitaji yao.

“Halmashauri zihakikishe vijana walio tayari kujihusisha na shughuli za uwekezaji wanapata taarifa za fursa za mitaji. Nyote mlimsikia Mheshimiwa Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akisisitiza kuhusu kutoa taarifa kwa walengwa,” alisema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa aliitaka mikoa iandae utaratibu wa kutoa elimu mtambuka kwa vijana ili wapate stadi za maisha na kufanya maamuzi sahihi na kusisitiza na utunzaji wa mazingira na mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI, maadili, uzalendo, mapambano dhidi ya dawa za kulevya na rushwa kupewa kipaumbele.      

Alieleza imani yake kwa vijana  walioshiriki  kongamano hilo kuwa  wameiva na wako tayari kwa kazi hivyo watumie maarifa waliyoyapata kuchangamkia fursa zilizopo ndani na nje ya Mkoa wa Dodoma na zaidi kuwa wadadisi kubaini na kuchangamkia fursa hizo.

”Mmeshapata maarifa mengi kupitia kongamano hili, wakati umefika sasa mnakwenda kutumia maarifa hayo kwa vitendo. Mikoa nayo iandae utaratibu wa kutoa elimu kuhusu masuala muhimu na mahsusi ya mtambuka kwa vijana ili wapate stadi za maisha na kufanya maamuzi sahihi.

“Nitoe wito kwenu vijana kuitumia fursa hii muhimu na adhimu mliyoipata katika kongamano hili kuanzisha na kuendeleza miradi yenu na baadaye kuondoa tatizo la ajira na umaskini kwa nchi yetu. Muhimu ni kuthubutu, kuchukua hatua, kuanza kidogo na kukua,” alisema.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alisema kongamano hilo la siku mbili limeshirikisha vijana zaidi ya 3,000 kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dodoma limelenga kuwawezesha vijana  kutambua fursa za kiuchumi zilizoko na kuzichangamkia

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...