WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, wakati wa kufunga kongamano la siku mbili la vijana wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Agosti 8, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa bidhaa ya gypsum na Meneja wa Taasisi ya Goldel Deco, Idd Abas wakati wa kufunga kongamano la siku mbili la vijana wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Agosti 8, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Dinna Charles akimuonyesha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mapambo yanayotengenezwa na Mfuko wa Tanzania Health Awareness and Support Foundation, wakati wa kufunga Kongamano la siku mbili la vijana wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Agosti 8, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia bidhaa tofauti tofauti zilizotengenezwa na vijana waliyonufaika na mkopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, kwenye kufunga Kongamano la siku mbili la vijana ambalo limewakutanisha vijana wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma, katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Agosti 08, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono Msanii mwenye ulemavu wa macho Joseph Hosea (kulia), kwenye kufunga Kongamano la siku mbili la vijana ambalo limewakutanisha vijana wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma, katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Agosti 08, 2023. Wapili kushoto ni Msanii Grace Maneno na wapili kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa hotuba ya kufunga kongamano la siku mbili la vijana wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Agosti 8, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)