HABARI PICHA
WATAALAMU wa Mfumo wa Anwani za Makazi (NaPA) Kitaifa kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakishiriki kikao cha pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) chenye lengo la kuweka mikakati ya pamoja ya kusajili Anwani za Makazi katika Hifadhi za Taifa ili kuboresha shughuli za utalii.
Kikao hicho kilifanyika Agosti 27, 2024 ofisi za Makao Makuu ya TANAPA, jijini Arusha.
.