MAJALIWA AKAGUA UJENZI MJI WA SERIKALI

Date:

Share post:

*Aagiza ifikapo Oktoba mwaka huu uwe umekamilika

RIPOTA WA WAZIRI MKUU

Dodoma

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi wanaojenga majengo ya Serikali katika Mji wa Serikali yaliyopo Mtumba jijini Dodoma kukamilisha kazi hiyo ifikapo Oktoba, mwaka huu.

Amewataka wakandarasi hao kununua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyopo nchini ili kuokoa fedha za kigeni na kuongeza tija katika uwekezaji.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo baada ya kukagua ujenzi wa Mji wa Serikali na Uwanja wa Mashujaa, Mtumba jijini Dodoma. 

“Dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona watumishi wote waliohamia Dodoma wanafanya kazi kwenye majengo rasmi.

“Tafuteni mbinu za kiufundi za kukamilisha majengo haya kwa wakati bila kuathiri viwango ikiwa ni pamoja na kusimamia ujenzi huu usiku na mchana, tunataka tumalize majengo haya, Watanzania wanataka kuona majengo yanakamilika na kutumika,” amesema Majaliwa.

Wakati huo huo, Majaliwa amewataka wasimamizi wa ujenzi wa mradi huo watumie bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyopo nchini. 

“Rais Samia amesisitiza kuhusu uwekezaji na amekuwa akialika wawekezaji wa nje na wa ndani kujenga viwanda vya bidhaa mbalimbali hapa nchini ikiwemo marumaru (tiles). Tutumie bidhaa zao badala ya kuagiza bidhaa hizo kutoka nje,” amesema.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema mbali na mradi wa ujenzi wa majengo ya wizara pia mradi mwingine unaotekelezwa katika eneo hilo ni ujenzi wa uwanja wa Mashujaa ambao utakuwa na mnara utakaoongoza kwa urefu barani Afrika. Mnara huo utakuwa na urefu wa mita 110.

Awali, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Dk. Jim Yonazi alisema watahakikisha wanasimamia kikamilifu ujenzi wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili.

“Ifikapo Septemba 30, 2023 mradi huo utakuwa umekamilika,” alisema.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...