SAVARA AACHIA ALBAMU YAKE YA ‘SAVAGE LEVEL’

Date:

Share post:

 JOSEPH  SHALUWA

MSANII kutoka Kundi la Sauti Sol la nchini Kenya, Savara ameachia albamu yake aliyoipa jina la Savage Level sambamba na kutambulisha ngoma nyingine kutoka katika albamu hiyo iitwayo Sababisha.

Albamu hiyo ya Savara ina jumla ya nyimbo 14 ambazo zote ameziandaa na ‘kuziprodyuzi’ mwenyewe, zikiwa na mchanganyiko wa maudhui mbalimbali katika jamii ikiwemo mapenzi, elimu ya kiroho, ukuaji, matatizo ya msongo wa mawazo na kadhalika.

Kabla ya kuachia albamu hiyo, tayari Savara alishaanza kufanya poa kama solo artist nje ya Kundi la Sauti Sol baada ya kuachia ngoma kama Balance na Killem Everybody ambazo zimepokelewa vyema ndani na nje ya Afrika Mashariki.

Katika albamu yake hiyo, Savara ameshirikiana na wasanii Karun kwenye wimbo wa Vibration na Nyashinski katika ngoma ya More Than A Friend huku akielezea kwamba kilichomsukuma kuandika ngoma yake ya Sababisha, ni jinsi uhusiano wake na mama yake ulivyokuwa tangu alivyomzaa na jinsi alivyohangaika kumlea mpaka kuwa mtu mzima.

Akiingumzia albamu ya Savage Level, Savara amesema: “Hii ni zaidi ya chakula cha ubongo, inakupa nguvu ya kubadilisha mtazamo wa maisha yako kwenda kwenye uhalisia.

Kila mmoja anazo nguvu ndani yake ambazo zinaweza kumfanya kuwa mtu bora, katika albamu hii nimejaribu kumuonesha kila mtu namna ya kuzifikia nguvu hizo.”

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

NEWCASTLE KUMUUZA MSHAMBULIAJI WA BEI MBAYA

LONDON, UingerezaKLABU ya Newcastle United itampiga bei straika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Yoane Wissa,...

LIVERPOOL NAYO YAJITOSA KWA WHARTON

MERSEYSIDE, UingerezaLIVERPOOL imeungana na klabu zingine kubwa za Ulaya zinazomtolea macho kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton. Mtandao wa...

SINTOFAHAMU KUELEKEA MAZUNGUMZO YA PILI KATI YA MAREKANI, IRAN

WASHINGTON DC, MarekaniAKIZUNGUMZA na waandishi wa habari Aprili 16, 2026, Rais wa Marekani, Donald Trump, alisema ana matumaini...

TAJIRI WA MAN CITY ANAHUSIKA VIPI VITA NCHINI SUDAN?

MANCHESTER, UingerezaMMILIKI wa klabu ya Manchester City, Sheikh Mansour bin Zayed Al-Nahyan, anakabiliwa na tuhuma nzito za kusambaza...