Tuesday, December 24, 2024
spot_img

MTANGAZAJI MICHEZO APAMBANA KUMNUSURU BOSS TPA MPENDA RUSHWA YA NGONO

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

SHAFFIH Dauda, mtangazaji wa michezo na pia mchambuzi wa soka, ameanza kupambana ili kumnusuru Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Gabriel Mwita Thobias anayekabiliwa na skendali ya rushwa ya ngono na kunyanyasa wanawake sehemu za kazi.

Katika mapambano hayo aliyoyaanzisha ya kumpigania Thobias aliyesema ni kaka yake, Dauda alieleza kuwa yeye mwenyewe, Thobias na familia nzima wapo tayari kutekeleza chochote watakachoelekezwa ili mradi tu habari za skendali za Thobias zisiandikwe na zilizokwishaandikwa zifutwe mara moja.

Machi 12, 2022 majira ya saa 2 usiku, Dauda aliipigia simu Tanzania PANORAMA Blog na kujitambulisha kisha akaomba kuonana na mwandishi mahali popote atakapoelekezwa ili kulimaliza jambo hilo.

Alisema habari za Thobias kuomba rushwa ya ngono na kunyanyasa wanawake mahali pa kazi zimemvua nguo na sasa amechutama akiwa tayari kutekeleza atakachotakiwa na kwamba familia na vigogo wengine wapo tayari kumsaidia kutekeleza kitakachotakiwa ili habari hizo zikome.

“Shafii hapa, Dauda. Dauda ni mmoja tu kaka hapa mjini, habari za siku kwanza. Nimekupigia kaka mkubwa maana wewe ni mwenzangu katika tasnia, familia imenipa jukumu la kuongea na wewe kuhusu suala na bro wetu la hizi story za kuomba rushwa ya ngono.

“Kaka nisikilize, mtu mzima akivuliwa nguo huchutama, mimi huyo ni bro wangu unayemvua nguo, umemvua kabisa nguo. Hapa tulikuwa na kikao cha familia ndiyo kimemalizika. Bro anaomba na familia inaomba, yupo tayari kwa lolote utakalosema na familia na wakubwa watamuunga mkono kutekeleza utakachosema ili hili liishe.

“Niamini mimi, bro yupo tayari kabisa kubadilisha maisha yako sema tu unataka nini na mimi mwenyewe nasimamia shoo, nambie upo wapi nije bro, nakuja kamili hakuna kubabaishana,” alisema Dauda.

Alipoulizwa anajua anaongea na nani alisema anajua kwa sababu wamefanya uchunguzi na kumbaini mmiliki wa Blog kabla yeye hajapewa jukumu la kukutana naye.

“Najua kaka, nakujua sana, kwani kuna mtu asiyemfahamu Simba? Nadhani umejua sasa nakujua maana najua pia unaitwa Simba. Hii blog yako inasomwa sana kwa sababu ni tofauti na zingine, wakubwa wanaipitia pitia sana kwa hiyo madhara ni makubwa kaka, hebu toa tamko kaka,” alisema Dauda.

Tanzania PANORAMA Blog iliamua kumpuuza Dauda kwa kumjibu kuwa inamkaribisha ofisini huku ikimweleza kuwa afike muda wa kazi akiwa na shida za kiofisi tu na si kupiga simu muda wa burudani.

Hata hivyo, Dauda hakukoma. Machi 13, 2022 majira ya saa 3.52 asubuhi kwa kutumia ukurasa wake wa whatsapp alituma ujumbe wa salamu na kijitambulisha kisha akakumbusha kuwa aliongea na PANORAMA usiku uliopita kuhusu suala la kaka yake.

Mjadala uliondelea baina ya PANORAMA na Dauda kwenye ukurasa wa whatsapp huu hapa chini.


Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya