![]() |
DCI Robert Boaz |
NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI wa Mashtaka (DCI) Robert Boaz amemkaribisha ofisini kwake, Govind Varsani Ravji wa Kampuni ya Ravji Construction Ltd anayemshtaki Murtaza Alihussein Dewji kwa kughushi nyaraka zenye saini yake na pia anayeilalamikia Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) kwa kujipatia fedha kwa njia ya udangannyifu (Utapeli)
Akizungumza jana na Tanzania PANORAMA Blog, iliyomuuliza kuhusu ofisi yake kutajwa kulikumbatia faili la kesi ya kughushi yenye nambari WH/IR/2657/2014 iliyofunguliwa Kituo cha Polisi Wazo Hill kisha ikafanyiwa uchunguzi na makachero wa kikosi cha uchunguzi wa makosa ya jinai, alisema ni vema mlalamikaji akafika ofisi za DCI ili apate maelezo kamili ya kinachoendelea.
DCI Boaz alisema hamfahamu mlalamikaji kwa sababu hajawahi kufika ofisini kwake na kwamba malalamiko anayoyatoa sasa anapaswa kwenda kuyatoa ofisini kwake ili apewe maelezo ajue hatua zilizofikiwa katika uchunguzi wa jambo hilo.
Alipoelezwa kuwa Tanzania PANORAMA Blog linaomba kujua hatua hizo alisema yeye ni mgonjwa hayupo ofisini lakini ofisi ipo, hivyo kama mlalamikaji atakwenda atakutana na maofisa ambao watazungumza naye.
“Mwambie aje ofisini, ….. hayo mambo atayafahamu vizuri akifika ofisini siyo kulalamika huko. Kama anasema anazungushwa pia nashangaa kwa sababu mimi sijawahi kukutana naye, simfahamu…… mimi sipo ofisini, ninaumwa, sijui nitakuwepo lini lakini ofisi ipo, mwambie aende ofisini atapewa maelezo ya kina kuhusu shauri lake… na wewe unaweza kuandika tu hivyo,” alisema DCI Boaz.
Taarifa zilizokusanywa na Tanzania PANORAMA Blog kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaki kuhusu mwenendo wa kesi hiyo zimeonyesha kuwa ni kweli jalada la kesi hiyo lilifikishwa katika ofisi hiyo na kufanyiwa kazi lakini Machi 2017 lilirudishwa ofisini kwa DCI baada ya kubainika lina upungufu unaopaswa kurekebishwa.
Wakati DCI akimkaribisha Ravji ofisini kwake, mlalamikaji huyo ameeleza kuwa kwa zaidi ya miaka minne amekuwa akizungushwa kila anapofuatilia mwenendo wa kesi hiyo ambayo tangu alipoifungua mwaka 2014 haijafikishwa mahakamani na mwaka 2016 alimwandikia barua ya wazi RaisDk. John Magufuli akimuomba aingilie kati kesi yake iweze kusikilizwa.
Barua hiyo iliyoandikwa kwa niaba yake na K.J Uisso inasomeka; ‘Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumelazimika kuandika barua hii ili kuleta malalamiko yetu kwako juu ya sintofahamu ya jalada la kesi husika, WH/IR/2657/2014, Murtaza s/o Dewji toka Wazo Hill Polisi Station, kughushi hati na saini.
‘Mheshimiwa Rais jalada hili lilipelekwa ofisi ya mwanasheria tangu tarehe 10/12/2014 lakini mpaka tunaandika barua hii shauri hili la jinai halijapelekwa mahakamani zaidi ya mtuhumiwa kutamba kuwa hakuna mtu wa kumfanya lolote kwani serikali ameiweka mfukoni.
‘Mnamo tarehe 27/01/2015, mwanasheria wa Kanda ya Dar es Salaam aliomba apewe siku mbili ili apeleke kesi mahakamani. Baada ya kusubiri kama alivyotuelekeza mwanasheria wa kanda tukavuta subira mpaka tarehe 12/02/2015. Hakuna kilichoendelea tukalazimika kupeleka malalamiko yetu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa barua ambayo niliwasilisha malalamiko yangu rasmi Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kueleza jinsi nilivyocheleshwa haki yangu tangu nimefungua jalada la uchunguzi katika kituo cha polisi Wazo Hill, Mei 2014.
‘Ofisi ya DPP ilinijibu barua yangu tarehe 13/03/2014 yenye kumb, Na AGC/PP/C.110/54/29 ambayo walikiri kupokea na wanayafanyia kazi malalamiko yangu na ufumbuzi ukipatikana watanijulisha.
‘Terehe 23/04/2015 niliandikiwa barua nyingine na Mkurugenzi E. Kakolaki yente Kumb. Na. AGC/PP/c.110/54/37 na kueleza kubainika kwa mapungufu kwenye hilo jalada hivyo tarehe 15/02/2015 faili lilirudishwa polisi.
‘Tarehe 14/09/2015 niliandikiwa barua nyingine yenye Kumb. Na.ABC/PP/C.190/36104/17 kunijulisha kuwa kosa lenyewe ni kubwa hivyo ni vema upelelezi ukafanywa kwa umakini mkubwa na kwamba niedelee kuvuta subira. Iliandikwa na M. Mchungahela.
‘Mheshimiwa Rais baada ya kuona mwaka wa pili na nusu umeisha nikaona ni vema niwakumbushe tena kwa barua yangu ya tarehe 04/01/2016 Kumb. Na. RCL/Mbezi/Plot105/56 na kuwaeleza kuhusu haki yangu inavyocheleshwa kwani inaonekana inapotea. Nilijibiwa kwa barua ya terehe 28/10/2016 yenye Kumb. Na. ACG/PP/C190/3/04/21 ambayo inaeleza upelelezi unachukua muda mrefu kwa sababu unahusisha vyombo vingine zaidi ya Polisi na kwamba File liko kwa Mkurugnzo wa Makosa ya Jinai (DCI)
‘Mh. Rais mpaka hivi leo tunaandika barua hii hatujaona juhusi zozote za kufikisha suala hli mahakamani zaidi ya kuzungushwa na watendaji hasa wakurugenzi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Divisheni ya Mashitaka.
‘Mheshimiwa Rais tunaomba ofisi yake itusaidie kutumbua hiki kijipu.’