RAIS SAMIA ATAJWA MAFANIKIO TANROADS

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo katika mwaka huu wa fedha 2022/23.

Mhandisi Mativila ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika mkutano wake na wanahabari uliojikita kuelezea mafanikio ya TANROADS ambayo imekuwa mstari wa mbele katika usimamizi wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya ujenzi wa barabara, madaraja na viwanja vya ndege.

Mhandisi Mativila amesema tangu kuanzishwa kwake, TANROADS imeweza kusimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara kuu na za Mikoa zenye urefu wa kilometa 36,362.

“TANROADS imekuwa na mipango mingi ili kuhakikisha nchi inakuwa na barabara nyingi za lami ikiwemo kushirikiana na sekta binafsi kwa ajili ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami,” ameeleza.

Aidha, alisema kumekuwa na mafanikio makubwa ya ujenzi wa madaraja na viwanja vya ndege chini ya uongozi wa Rais Samia kwakuwa amekuwa mstari wa mbele kwa kutoa fedha kwa wakati na maelekezo bora yaliyokuwa na ufanisi kwao.

Amesema TANROADS ilianzishwa kwa Waraka wa Serikali uliotolewa katika gazeti la Serikali Na. 293 la tarehe 25 Agosti, 2000 kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya Mwaka 1997.

Malengo ya kuanzishwa kwa Tanroads ni kuleta ufanisi zaidi katika majukumu yaliyokuwa chini ya Idara ya Barabara ndani ya Wizara ya Ujenzi.

Habari Leo

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...