Tuesday, December 24, 2024
spot_img

SAMIA AONYA UDOKOZI MIRADI YA UMMA

RIPOTA PANORAMA

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania watakaopata fursa za ajira katika ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini hapa kuepuka udokozi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumapili Oktoba 30, 2022, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa uwanja huo.

Rais Samia amesema mradi huo ni mali ya Watanzania na wakazi wa Dodoma wote.

Rais Samia amewaomba Watanzania kutohujumu mradi huo na badala yake kuwa walinzi wake.

“Wakati mwingine mnapata ajira katika miradi hii lakini mnatabia ya mkono, mkono, kuondoka na mifuko ya saruji, kuondoka na kifuko cha misumari, kipande cha nondo.

“Niombe sana mtakaopata ajira hapa, twendeni tuwajibike ipasavyo ili mradi ukamilike Desemba 2024 wakati ,”amesema.

Amesema ujenzi wa viwanja vya ndege umepewa kipaumbele katika sera ya usafiri nchini ambapo kila mkoa unatakiwa kuwa na kiwanja cha ndege chenye uwezo wa kuhudumia ndege zinazobeba si chini ya abiria 70.

Amesema pamoja na uwanja wa ndege wa Msalato kuna viwanja vya ndege vingine vinaendelea kujengwa nchini.

Rais Samia amesema lengo lao ni kukuza biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya