‎Rais wa Real Madrid, Florentino Pérez, ameeleza kufurahishwa na mchango wa kocha José Mourinho katika kuijenga upya klabu hiyo na kuirejeshea ari ya ushindani kwenye ligi.

‎Pia Pérez amesema Mourinho alikuwa na nafasi kubwa katika kuunda utamaduni wa ushindani uliowezesha Real Madrid kufikia mafanikio makubwa katika miaka iliyofuata, ikiwemo kutwaa mataji sita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

‎Aidha kiongozi huyo amesisitiza kuwa Mourinho alikuwa mtu muhimu sana katika historia ya mafanikio ya klabu hiyo na anaamini ana uwezo wa kurejesha tena ari ya ushindani ndani ya kikosi cha Real Madrid.

‎Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka kuhusu uwezekano wa Mourinho kurejea kuinoa Real Madrid katika siku zijazo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here