FEI TOTO KUVUNJA REKODI YA MIAKA MINNE LIGI KUU BARA?

Date:

Share post:

TANGU George Mpole alipotwaa tuzo ya Mfungaji Bora Ligi Kuu Bara mwaka 2022, hakuna mchezaji mzawa aliyeweza kufanya hivyo hadi sasa, lakini kiungo wa Azam, Feisal Salum ‘Fei Toto’, huenda akaivunja rekodi hiyo msimu huu.

Fei Toto ndiye kinara wa mabao kufikia hatua hii ya msimu wa 2025-26, akiwa ameingia kambani mara 10, achilia mbali ‘asisti’ zake saba.

Itakumbukwa, Mpole akiwa na Geita Gold, alifunga mabao 17 alipotwaa kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2021-22, wakati huo Fei Toto akiwa amezifumania nyavu mara sita pekee.

Tangu wakati huo, wachezaji wa kigeni wamekuwa wakipokezana tuzo hiyo, huku washambuliaji wazawa wakiishia kuwa wasindikizaji tu.

Mastaa wa kigeni walioibuka wafungaji bora kwa misimu mitatu mfululizo ya hivi karibuni ni pamoja na Ahoua wa Simba aliyefanya hivyo msimu uliopita (2024-25) akiwa na mabao 16.

Wengine ni Stephanie Aziz Ki (mabao 21, 2023-24) na Fiston Mayele (mabao 16, 2022-23), wote wakipata heshima hiyo wakiwa na Yanga.

Msimu wa 2023-24, Fei Toto alikaribia kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara lakini mabao yake 19 hayakutosha mbele ya Aziz Ki aliyebeba tuzo hiyo kwa tofauti ya mabao mawili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MLANGO-BAHARI WA HORMUZ UNAVYOITESA DUNIA

TEHRAN, Iran MGOGORO unaoendelea kati ya Iran na Marekani katika Mlango-Bahari wa Hormuz umetikisa uchumi wa dunia. Kila nchi,...

MWAKA MMOJA WA PAPA LEO AKIIONGOZA VATICAN

WASHINGTON DC, Marekani UMETIMIA mwaka mmoja tangu Papa Leo XIV alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki duniani. Aliingia madarakani Mei 8,...

STEVE BARKER AMEANZA KUJIPATA LIGI KUU BARA

UKIFUATILIA msimamo wa Ligi Kuu Bara na kiwango cha Simba katika mechi za hivi karibuni, unaweza kusema sasa...

WAZIRI WA IRAN AINYOOSHEA KIDOLE MAREKANI

TEHRAN, Iran NI Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ambaye ameitupia lawama Marekani akisema imekuwa ikitibua...