SERIKALI KUIMARISHA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, KUPANUA FURSA ZA MIKOPO

Date:

Share post:

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kuimarisha uwezeshaji wanawake kiuchumi pamoja na kuongeza uelewa kuhusu mifuko ya maendeleo inayowanufaisha wanawake nchini.

Akizungumza Mei 6, 2026 bungeni jijini Dodoma, Mhe. Mahundi amesema Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wanawake wengi zaidi wanapata taarifa sahihi na kunufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) huku akisistiza miongoni mwa mikakati hiyo ni kushirikiana na taasisi za fedha na wadau wa maendeleo kutoa mafunzo ya ujasiriamali na uendeshaji wa biashara kupitia makongamano ya kikanda.

“Serikali itaendelea kushirikiana na Wizara ya Fedha, TAMISEMI pamoja na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuhakikisha makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu yanapatiwa mafunzo na fursa za mikopo nafuu,” amesema Mhe. Mahundi.

Katika hatua nyingine, ameeleza kuwa Serikali imejikita zaidi katika kuimarisha mifuko iliyopo badala ya kuanzisha mipya, ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake unaotoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake wajasiriamali.

Aidha, amesema kupitia ushirikiano na Benki ya Dunia, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuanza utoaji wa mikopo kupitia mradi wa PAMOJA, hatua itakayopanua wigo wa wanawake kunufaika na fursa za kiuchumi.

Mhe. Mahundi amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi, taasisi za fedha pamoja na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha wanawake wanajengewa uwezo wa kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

ATHARI ZA VITA MASHARIKI YA KATI: BEI YA MAFUTA YAZIDI KUPAA NCHINI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za kikomo za mafuta ya...

BAHARIA MTANZANIA AFARIKI DUNIA BAADA YA MELI KUSHAMBULIWA MLANGO BAHARI WA HORMUZ

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limethibitisha kifo cha baharia raia wa Tanzania, Mchama Maregesi Mongu, aliyefariki...

WANNE WANASHIKILIWA KWA MAUAJI YA MWANAFUNZI WA IFM

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne wanaohusishwa na tukio la mauaji ya...

BAHI YA TUMIA MICHEZO KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mashindano...