WANNE WANASHIKILIWA KWA MAUAJI YA MWANAFUNZI WA IFM

Date:

Share post:

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne wanaohusishwa na tukio la mauaji ya mwanafunzi James Temba wa mwaka wa pili katika Chuo cha IFM.

Watuhumiwa hao ni Steven Chaka (31) Afisa maabara mkazi wa Bomang’ombe, Hai mkoani Kilimanjaro, Anna Lema maarufu kama Happiness (30) mfanyabiashara mkazi wa Tabata Chang’ombe, Twalibu Khamis maarufu kama Mputo (23) mkazi wa Kigogo Kati na Michael John maarufu kama Tambali (26) pia mkazi wa Kigogo Kati.

Tukio hilo lilitokea Aprili 30, 2026, ambapo mwili wa James Temba ulipatikana unaelea katika maji ya Mto Msimbazi eneo la Kipawa, Ilala ukiwa hauna kichwa.

Polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi wa kina wa tukio hilo, na kwamba baadhi ya vielelezo muhimu vinaendelea kuchunguzwa ili kubaini ukweli wa kilichotokea.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema uchunguzi huo unafanyika kwa uzito mkubwa na kwamba kila atakayebainika kuhusika atachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha, Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea.

Mwili wa marehemu James Temba umeaagwa leo jijini Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwenda Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SERIKALI KUIMARISHA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, KUPANUA FURSA ZA MIKOPO

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali inaendelea...

ATHARI ZA VITA MASHARIKI YA KATI: BEI YA MAFUTA YAZIDI KUPAA NCHINI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za kikomo za mafuta ya...

BAHARIA MTANZANIA AFARIKI DUNIA BAADA YA MELI KUSHAMBULIWA MLANGO BAHARI WA HORMUZ

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limethibitisha kifo cha baharia raia wa Tanzania, Mchama Maregesi Mongu, aliyefariki...

BAHI YA TUMIA MICHEZO KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mashindano...