BAHI YA TUMIA MICHEZO KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Date:

Share post:

Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mashindano ya michezo yaliyopewa jina la “Nishati Safi Cup”, yakihusisha vijiji 16 kutoka katika kata 8 za wilaya hiyo.

Mashindano hayo, ambayo yataendelea kwa takribani miezi miwili, yanalenga kuunganisha burudani na elimu kwa jamii ili kufikisha ujumbe kuhusu matumizi ya nishati salama, nafuu na rafiki kwa mazingira.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Francis Kasambala, amesema kupitia mashindano hayo elimu inatolewa kwa njia shirikishi zaidi inayowafikia wananchi wengi kwa urahisi.

Amesema sambamba na michezo, timu ya wataalamu inaendelea kutembelea shule mbalimbali na kuendesha midahalo kwa wanafunzi, lengo likiwa ni kuwajengea uelewa kuhusu faida za matumizi ya nishati safi tangu wakiwa katika umri mdogo.

“Tunatumia michezo kama jukwaa la kuelimisha jamii. Kupitia Nishati Safi Cup, tunafikia wananchi wengi zaidi huku tukihamasisha mabadiliko ya tabia katika matumizi ya nishati ya kupikia. Hii ni njia ya vitendo inayosaidia ujumbe kueleweka kwa urahisi,” amesema Kasambala.

Aidha, wananchi mbalimbali wakiwemo wachoma nyama na wafanyabiashara wadogo wamepatiwa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mikutano ya hadhara na matukio yanayoambatana na mashindano hayo. huku Elimu hiyo ikilenga kuwasaidia nakutoa uelewa kuhusu faida za kutumia nishati safi katika shughuli zao za biashara, hususan kupunguza gharama na kulinda mazingira.

Kwa upande wake, mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati, Kitengo cha Nishati Safi ya Kupikia, Benezeth Kabunduguru, amesema Serikali inaendelea kutoa elimu sambamba na kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwawezesha wananchi kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Ameongeza kuwa matumizi ya nishati safi si tu yanapunguza athari za mazingira, bali pia yanaboresha afya za wananchi na kupunguza muda na gharama zinazotumika katika shughuli za kupikia,huku akisisitiza kuwa kampeni kama hizi za jamii ni muhimu katika kuharakisha mabadiliko ya tabia nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RC MAKALLA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA NA BARABARA ZA AFCON ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Gabriel Makalla amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo...

RUTO ATAJA UWEKEZAJI WA KENYA TANZANIA KUFIKIA DOLA BILIONI 1.7, AONYA URASIMU MIPAKANI

Rais wa William Ruto amesema kuwa takribani kampuni 500 kutoka Kenya zimewekeza jumla ya dola za Marekani bilioni...

RUTO ASISITIZA USHIRIKIANO WA EAC NI UFUNGUO WA KUKUZA BIASHARA NA AJIRA KWA WANANCHI

Rais wa William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zina fursa kubwa ya kuongeza biashara ya ndani na...

WIZARA YA MAJI KUIMARISHA TEKNOLOJIA KUDHIBITI UPOTEVU WA MAJI NCHINI

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema Wizara yake itaendelea kuimarisha udhibiti wa upotevu wa maji katika mifumo ya...