WANANCHI ZAIDI YA MILIONI 15 KUNUFAIKA NA TEKNOLOJIA YA KAMERA ZA FUNDUS

Date:

Share post:

Zaidi ya wananchi milioni 15 hadi 20 wanatarajiwa kunufaika na matumizi ya teknolojia ya Kamera za Fundus (Portable Fundus Camera) zitakazotumika kubaini mapema athari za ugonjwa wa Kisukari kwenye macho, hususan tatizo la Diabetic Retinopathy.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Edith Bakari, wakati wa mafunzo ya matumizi ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, ambapo Amesema teknolojia hiyo italenga kuwahudumia wananchi wa mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya na maeneo ya jirani.

Ameongeza kuwa matumizi ya kamera hizo yatawezesha kugundua mapema athari za kisukari kwenye macho kabla ya kufikia hatua hatarishi, hatua itakayosaidia kuanza matibabu kwa wakati na hivyo kupunguza au kuzuia kabisa upofu unaoweza kuepukika.

“Vifaa hivi vitatumika kikamilifu katika kliniki za wagonjwa wa kisukari zilizopo hospitalini pamoja na huduma za mkoba, jambo litakalosaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi wasioweza kufika kirahisi vituo vya afya,” amesema Bakari.

Aidha, ameishukuru London School of Hygiene and Tropical Medicine (LSHTM) kwa ushirikiano wake wa karibu na Wizara ya Afya katika kuboresha huduma za macho nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho, Dkt. Eunice Headcraph, amesema baada ya mafunzo hayo, wataalamu kutoka hospitali zilizopokea vifaa hivyo ikiwemo Hospitali ya Benjamin Mkapa, Hospitali ya Muhimbili Mloganzila na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wanatarajiwa kuanza mara moja kutoa huduma hiyo.

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa wataalamu hao kutumia kikamilifu vifaa hivyo na kuhakikisha wanawasilisha taarifa za utekelezaji kila mwezi, zikionesha idadi ya wagonjwa waliopatiwa huduma, waliogundulika na changamoto pamoja na aina ya matibabu yaliyotolewa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

BAHI YA TUMIA MICHEZO KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mashindano...

RC MAKALLA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA NA BARABARA ZA AFCON ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Gabriel Makalla amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo...

RUTO ATAJA UWEKEZAJI WA KENYA TANZANIA KUFIKIA DOLA BILIONI 1.7, AONYA URASIMU MIPAKANI

Rais wa William Ruto amesema kuwa takribani kampuni 500 kutoka Kenya zimewekeza jumla ya dola za Marekani bilioni...

RUTO ASISITIZA USHIRIKIANO WA EAC NI UFUNGUO WA KUKUZA BIASHARA NA AJIRA KWA WANANCHI

Rais wa William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zina fursa kubwa ya kuongeza biashara ya ndani na...