SERIKALI YAPIGA HATUA UTOAJI HUDUMA ZA MAJI KWA WANANCHI NCHINI

Date:

Share post:

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema Serikali imeendelea kupiga hatua kubwa katika kuboresha huduma ya maji safi na salama nchini, huku ikiweka lengo la kufikia upatikanaji wa asilimia 90 vijijini na asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2030.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2026/2027 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma Mei 5, 2026, Aweso alisema hadi Desemba 2025 upatikanaji wa maji vijijini umefikia wastani wa asilimia 85.2 kutoka asilimia 83.1 mwaka 2024.

Ameeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na kukamilika kwa miradi 54 yenye vituo 946 vya kuchotea maji, iliyowanufaisha wananchi 493,932 katika vijiji 151, na hivyo kufanya jumla ya wananchi wa vijijini wanaopata huduma hiyo kufikia zaidi ya milioni 38.6.

Kwa upande wa mijini, Waziri Aweso alisema hali ya upatikanaji wa maji imefikia asilimia 92.5 hadi Desemba 2025, ikilinganishwa na asilimia 90.6 mwaka uliopita. Amebainisha kuwa mafanikio hayo yametokana na kukamilika kwa miradi 12 inayohudumia zaidi ya watu 880,000, huku miradi mingine 214 ikiendelea kutekelezwa.

Katika hatua nyingine, Aweso alitoa maelekezo mazito kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji nchini kuhakikisha wanawarejeshea huduma ya maji wateja wote waliokatwa kutokana na kushindwa kulipa faini.

Aidha, ametoa onyo kali kwa baadhi ya mamlaka hizo kwa tabia ya kubambikizia wateja bili kubwa zisizoendana na matumizi halisi, akisisitiza kuwa vitendo hivyo ni unyanyasaji kwa watumiaji na havikubaliki katika Serikali ya Awamu ya Sita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

BAHI YA TUMIA MICHEZO KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mashindano...

RC MAKALLA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA NA BARABARA ZA AFCON ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Gabriel Makalla amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo...

RUTO ATAJA UWEKEZAJI WA KENYA TANZANIA KUFIKIA DOLA BILIONI 1.7, AONYA URASIMU MIPAKANI

Rais wa William Ruto amesema kuwa takribani kampuni 500 kutoka Kenya zimewekeza jumla ya dola za Marekani bilioni...

RUTO ASISITIZA USHIRIKIANO WA EAC NI UFUNGUO WA KUKUZA BIASHARA NA AJIRA KWA WANANCHI

Rais wa William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zina fursa kubwa ya kuongeza biashara ya ndani na...