EMERY ATAJWA KUCHUKUA MIKOBA REAL MADRID

Date:

Share post:

MADRID, Hispania

KOCHA anayefanya vizuri Ligi Kuu ya England (EPL) akiwa na kikosi cha Aston Villa, Unai Emery, anafukuziwa na Real Madrid.

Emery bado ana mkataba na Villa unaotarajiwa kufikia ukomo mwaka 2029. Alijiunga na timu hiyo mwaka 2022.

Madrid wanasaka kocha mpya kwa ajili ya msimu ujao, ambaye atachukua mikoba ya Alvaro Arbeloa anayetarajiwa kuachia ngazi mwishoni mwa msimu huu.

Kwa upande wake, Emery si jina geni Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga), ambapo aliwahi kuzinoa Almeria, Valencia, Sevilla na Villarreal.

Pia, kama itakumbukwa, kwa nyakati tofauti aliwahi kufanya kazi kwenye mabenchi ya ufundi ya klabu za Arsenal na PSG.

Katika hatua nyingine, Rais wa zamani wa Madrid, Ramon Calderon, amesema hana uhakika kama Emery ni chaguo sahihi kwa klabu hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

BAHI YA TUMIA MICHEZO KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mashindano...

RC MAKALLA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA NA BARABARA ZA AFCON ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Gabriel Makalla amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo...

RUTO ATAJA UWEKEZAJI WA KENYA TANZANIA KUFIKIA DOLA BILIONI 1.7, AONYA URASIMU MIPAKANI

Rais wa William Ruto amesema kuwa takribani kampuni 500 kutoka Kenya zimewekeza jumla ya dola za Marekani bilioni...

RUTO ASISITIZA USHIRIKIANO WA EAC NI UFUNGUO WA KUKUZA BIASHARA NA AJIRA KWA WANANCHI

Rais wa William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zina fursa kubwa ya kuongeza biashara ya ndani na...