RUTO ASISITIZA USHIRIKIANO WA EAC NI UFUNGUO WA KUKUZA BIASHARA NA AJIRA KWA WANANCHI

Date:

Share post:

Rais wa William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zina fursa kubwa ya kuongeza biashara ya ndani na kunufaika zaidi kiuchumi iwapo zitaimarisha ushirikiano wa kikanda.

Akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma leo Mei 5, 2026, Ruto amesema kiwango cha biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki bado ni kidogo, kikikadiriwa kuwa kati ya asilimia 15 hadi 30, hali inayoonyesha kuwa sehemu kubwa ya biashara inaendelea kufanyika nje ya ukanda huo.

Aidha ameongeza kuwa pamoja na changamoto hiyo, bado kuna fursa kubwa kwa nchi wanachama kuongeza biashara baina yao, hatua itakayosaidia kufungua masoko mapya, kuimarisha viwanda na kuongeza ajira kwa wananchi.

Rais Ruto amesisitiza kuwa vijana ndio chachu ya mafanikio ya ajenda hiyo, akieleza kuwa kila mwaka mamilioni ya vijana kutoka nchi za ukanda huo wanaingia kwenye soko la ajira wakiwa na vipaji, na ndoto kubwa ambapo vijana hao hawahitaji misaada bali wanahitaji fursa, akibainisha kuwa kwa kuimarisha ushirikiano wa kikanda, kuwekeza katika miundombinu ya pamoja na kupanua biashara, Afrika Mashariki inaweza kuwa kinara wa ajira, ujasiriamali na maendeleo endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

BAHI YA TUMIA MICHEZO KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mashindano...

RC MAKALLA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA NA BARABARA ZA AFCON ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Gabriel Makalla amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo...

RUTO ATAJA UWEKEZAJI WA KENYA TANZANIA KUFIKIA DOLA BILIONI 1.7, AONYA URASIMU MIPAKANI

Rais wa William Ruto amesema kuwa takribani kampuni 500 kutoka Kenya zimewekeza jumla ya dola za Marekani bilioni...

WIZARA YA MAJI KUIMARISHA TEKNOLOJIA KUDHIBITI UPOTEVU WA MAJI NCHINI

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema Wizara yake itaendelea kuimarisha udhibiti wa upotevu wa maji katika mifumo ya...