RUTO ATAJA UWEKEZAJI WA KENYA TANZANIA KUFIKIA DOLA BILIONI 1.7, AONYA URASIMU MIPAKANI

Date:

Share post:

Rais wa William Ruto amesema kuwa takribani kampuni 500 kutoka Kenya zimewekeza jumla ya dola za Marekani bilioni 1.7 nchini Tanzania, hatua ambayo imechochea ajira kwa mamilioni ya wananchi na kuongeza mapato ya serikali.

Akihutubia Bunge la Tanzania jijini Dodoma leo Aprili 5, 2026, Rais Ruto amesema uwekezaji huo umeonesha kuimarika kwa uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Kenya, na kwamba umeongeza fursa za kiuchumi kwa mataifa hayo mawili.

Ameeleza kuwa si Kenya pekee imewekeza Tanzania, bali pia kampuni za Kitanzania zimepanua shughuli zake nchini Kenya, akizitaja Taifa Gas, Amson Group na Lake Gas kuwa miongoni mwa wawekezaji wakubwa.

Aidha Amebainisha kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu, uwekezaji huo umeendelea kuchochea ukuaji wa uchumi wa pande zote mbili, na amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji wa kikanda.

“Niliwaambia Wakenya kuwa mwekezaji kutoka Tanzania ni mshirika wetu; wanatuletea mitaji na fursa za ajira.”Amesema Ruto

Hata hivyo, Rais Ruto ameonya tabia za kiburi na jeuri miongoni mwa baadhi ya watumishi wa serikali, hususan waliopo mipakani ambazo zimekuwa zikikwamisha biashara na kusababisha upotevu wa mabilioni ya fedha huku akiongeza kuwa vikwazo visivyo vya lazima na mienendo isiyo rafiki kwa wafanyabiashara vinaendelea kudhoofisha biashara ya mipakani na kupunguza ufanisi wa sekta binafsi.

Mbali nahayo Amesisitiza kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC zinapaswa kuchukua hatua za makusudi kuondoa urasimu na kurahisisha mifumo ya biashara ili kukuza uchumi wa kikanda.

Kwa ujumla , ziara ya Rais Ruto ilianza jana mei 4 nchini Tanzania ambapo amekutana na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan imezaa makubaliano makubwa ya kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi na kusaini mikataba nane katika sekta za nishati, miundombinu, ulinzi na TEHAMA.

Pia, nchi hizo zimekubaliana kuendeleza miradi ya kimkakati ikiwemo kuunganisha umeme, ujenzi wa bomba la gesi kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa, pamoja na kuimarisha reli na usafiri wa majini katika Ziwa Victoria, hatua inayotarajiwa kuongeza biashara na kukuza uchumi wa kikanda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

BAHI YA TUMIA MICHEZO KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mashindano...

RC MAKALLA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA NA BARABARA ZA AFCON ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Gabriel Makalla amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo...

RUTO ASISITIZA USHIRIKIANO WA EAC NI UFUNGUO WA KUKUZA BIASHARA NA AJIRA KWA WANANCHI

Rais wa William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zina fursa kubwa ya kuongeza biashara ya ndani na...

WIZARA YA MAJI KUIMARISHA TEKNOLOJIA KUDHIBITI UPOTEVU WA MAJI NCHINI

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema Wizara yake itaendelea kuimarisha udhibiti wa upotevu wa maji katika mifumo ya...