BAHARIA MTANZANIA AFARIKI DUNIA BAADA YA MELI KUSHAMBULIWA MLANGO BAHARI WA HORMUZ

Date:

Share post:

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limethibitisha kifo cha baharia raia wa Tanzania, Mchama Maregesi Mongu, aliyefariki dunia Mei 3, 2026 wakati akitekeleza majukumu yake katika meli ya kuvuta (tug boat) iitwayo VOLANS.

Kwa mujibu wa taarifa ya TASAC, meli hiyo iliyosajiliwa na Shirika la Usajili la Kimataifa wa Bahari (IMO Na. 9298566) na kubeba bendera ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), iliyokuwa ikisafiri kutoka UAE kuelekea Oman kabla ya kushambuliwa na bomu wakati ikipita katika Mfereji wa Hormuz, eneo linalounganisha nchi za Iran na Oman.

TASAC imetoa pole kwa familia, ndugu na marafiki wa marehemu kufuatia msiba huo mzito, huku ikiungana nao katika kipindi hiki cha majonzi.

Aidha, shirika hilo limesema linaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatilia kwa karibu tukio hilo, ikiwa ni pamoja na juhudi za kuurejesha mwili wa marehemu nchini mara utakapopatikana.

Katika hatua nyingine, TASAC imekumbusha umuhimu wa kulinda maisha ya mabaharia wanaofanya kazi katika maeneo hatarishi, ikisisitiza uzingatiaji wa haki ya kupita kwa amani (innocent passage) kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria za Bahari (UNCLOS).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SERIKALI KUIMARISHA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI, KUPANUA FURSA ZA MIKOPO

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali inaendelea...

ATHARI ZA VITA MASHARIKI YA KATI: BEI YA MAFUTA YAZIDI KUPAA NCHINI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za kikomo za mafuta ya...

WANNE WANASHIKILIWA KWA MAUAJI YA MWANAFUNZI WA IFM

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne wanaohusishwa na tukio la mauaji ya...

BAHI YA TUMIA MICHEZO KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mashindano...