MWAKA MMOJA WA PAPA LEO AKIIONGOZA VATICAN

Date:

Share post:

WASHINGTON DC, Marekani

UMETIMIA mwaka mmoja tangu Papa Leo XIV alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki duniani. Aliingia madarakani Mei 8, 2025.

Hata hivyo, kwa miezi 12 aliyokaa Vatican, Papa Leo ameonesha kufuata nyayo za watangulizi wake, akiwamo Papa Francis, ingawa pia kuna utofauti.

Kwa muda wake mwingi, Papa Leo amekuwa akihimiza amani, kama ambavyo aliahidi wakati anaingia madarakani Mei 8, 2025.

Mtangulizi wake, Papa Francis, kama itakumbukwa, alikuwa mkosoaji mkubwa wa kile kinachoendelea Kati ya Urusi na Ukraine, pia vita vinavyozihusha Israel na Palestina kule Gaza.

Kwa upande wa Papa Leo, ajenda ya kutaka amani itawale duniani iliibua vita kali kati yake na Mmarekani mwenzake, Rais Donald Trump.

Ni baada ya Papa Leo kukosoa matendo ya uvunjifu ya vikosi vya Marekani katika nchi za Venezuela na Iran. Vita vya maneno viliongezeka zaidi baada ya Trump kutishia kuifuta Iran katika uso wa dunia.

Papa Leo aliibuka na kusema vitisho vya aina hiyo havikubaliki, na badala yake alisisitiza umuhimu wa diplomasia kutumika katika kutatua migogoro.

Hata hivyo, Rais Trump alimjia juu kiongozi huyo wa kiroho, akimtaka kuachana na siasa kwa kuwa hakuna analolijua. Alimshauri kujikita zaidi katika masuala ya dini.

Huku Papa Leo akisema hatishwi na utawala wa Rais Trump, vita vyao hivyo viliibua mijadala duniani kote.

Wengi walimtaja Rais Trump kuwa ni mtu aliyevuka mipaka, wakisema hata madiketa waliowahi kutikisa dunia, akiwamo Adolf Hitler, hawakuwahi kumvunjia heshima kiongozi wa Kanisa Katoliki.

Ni kutokana na uhusiano mbaya huyo, huenda Papa Leo, ambaye ni mzaliwa wa Chicago, asifanye ziara yoyote Marekani kipindi hiki Rais Trump akiwa madarakani.

Kwamba zile taarifa za Papa Leo kuhudhuria sherehe za uhuru Julai 4, 2026 ni porojo, na badala yake ataitumia siku hiyo akiwa katika Kisiwa cha Lampedusa.

Kwa upande mwingine, miezi 12 akiwa kiongozi wa Kanisa Katoliki imeshuhudia Papa Leo akilipa kipaumbele Bara la Afrika kuliko Ulaya.

Aprili, 2026, alitumia siku 11 kufanya ziara yake katika nchi nne za Afrika. Ni siku nyingi, ukilinganisha na miaka yote nane ya uongozi wa mtangulizi wake, Papa Francis.

Papa Leo anafahamu kuwa ushawishi wa Kanisa Katoliki barani Afrika huongezeka kwa asilimia hadi 30 kwa mwaka. Ni tofauti na Ulaya, ambako ushawishi wake unatajwa kuporomoka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MLANGO-BAHARI WA HORMUZ UNAVYOITESA DUNIA

TEHRAN, Iran MGOGORO unaoendelea kati ya Iran na Marekani katika Mlango-Bahari wa Hormuz umetikisa uchumi wa dunia. Kila nchi,...

STEVE BARKER AMEANZA KUJIPATA LIGI KUU BARA

UKIFUATILIA msimamo wa Ligi Kuu Bara na kiwango cha Simba katika mechi za hivi karibuni, unaweza kusema sasa...

FEI TOTO KUVUNJA REKODI YA MIAKA MINNE LIGI KUU BARA?

TANGU George Mpole alipotwaa tuzo ya Mfungaji Bora Ligi Kuu Bara mwaka 2022, hakuna mchezaji mzawa aliyeweza kufanya...

WAZIRI WA IRAN AINYOOSHEA KIDOLE MAREKANI

TEHRAN, Iran NI Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ambaye ameitupia lawama Marekani akisema imekuwa ikitibua...