NINI CHANZO MGOGORO WA UKRAINE, ISRAEL?

Date:

Share post:

KYIV, Ukraine

BAADA ya miaka mingi ya ukaribu na mahusiano mazuri, Ukraine na Israel zimeingia kwenye mgogoro wa kidipmolasia.

Chanzo cha mgogoro huo ni mwandishi wa habari, Kateryna Yaresko, ambaye anafanya kazi na Taasisi inayochunguza uhalifu dhidi ya Serikali ya Ukraine.

Kupitia ukura wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Yaresko alianzisha tatizo hilo Aprili 21, 2026, alipofichua juu ya ‘biashara ya siri’ kati ya Israel na Urusi.

Katika ripoti yake, mwandishi huyo alisema meli ya mizigo ya Urusi iliwasili katika bandari ya Israel ikiwa na tani 43,765.18 za nafaka aina ya ngano ilizoiba Ukraine.

Taarifa hiyo iliibua vita ya maneno kwa viongozi waandamizi wa pande zote mbili, kwa maana ya Ukraine na Israel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha, alikuwa wa kwanza kuzungumzia hilo wiki mbili tu baada ya ripoti ya mwandishi Yaresko.

Sybiha alisema meli nyingine ya Urusi iliyobeba nafaka zilizoibiwa Ukraine ilitia nanga katika moja ya bandari nchini Israel.

Alisema Ukraine ilishawasilisha ombi kwa Israel ikitaka iisaidie kuchunguza meli iitwayo Abinsk kwa madai kuwa imekuwa ikitumiwa na Urusi kusafirisha nafaka kutoka Ukraine.

Alisema: “Ni ngumu kuelewa kwanini Israel inashindwa kufanyia kazi ombi la Ukraine kutaka izuie bidhaa zinazoingizwa (kwa siri) mjini Haifa.”

Katika taarifa yake hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), Sybiha aliongeza kuwa Israel kuendelea kutumika katika wizi wa bidhaa za Ukraine kutaua mahusiano mazuri yaliyopo kati ya mataifa hayo.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Saar, naye alitumia jukwaa hilo la kidigitali kujibu, akisema: “Hakuna ushahidi wa kuthibitisha hilo.

“… Mahusiano ya kidipmolasia, hasa kwa nchi rafiki, hayaendeshwi kupitia Twitter au vyombo vya habari.”

Lakini, Saar alisisitiza kuwa mamlaka za Israel zitafanya uchunguzi na endapo zitabaini kuwapo kwa biashara hiyo, basi zitachukua hatua kali.

Kwa upande wake, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, naye ameingilia mzozo huo akisema: “Katika nchi yoyote, kununua bidhaa za wizi ni kosa la jinai na zipo adhabu zake. Ni kama ambavyo Urusi inaiba nafaka za Ukraine.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KISWAHILI KUIMARISHWA NCHINI KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili...

‘KARIAKOO DERBY’ YAVUNJA REKODI YA MABAO

BAADA ya sare ya mabao 2-2 jana Mei 3, 2026, mechi inayozikutanisha Simba na Yanga, maarufu kwa jina...

MASTAA WA KIGENI WAENDELEA KUTAMBA ‘KARIAKOO DERBY’

DAKIKA 90 za 'Kariakoo Derby' zilitamatika jana Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Jenerali Isamhuyo jijini Dar es...

PANYA, NGUCHIRO WANAVYOTESA RAIA WA PALESTINA UKANDA WA GAZA

JERUSALEM, Palestina NI katika kambi za raia wa Palestina wanaoishi kwenye mahema baada ya makazi yao kusambaratishwa na mashambulizi...