KATIKA mchezo wa kesho Mei 10, 2026 dhidi ya Simba, Tanzania Prisons itahitaji maajabu ya soka tu ili kupata ushindi. Ni kwa mujibu wa takwimu za ‘Wajelajela’ hao msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Prisons ya jijini Mbeya haijaonja usindi katika mechi nane mfululizo za Ligi Kuu, na badala yake imefungwa sita na kuambulia sare mbili.
Kwamba mara ya mwisho kwa timu hiyo kupata pointi tatu za mchezo mmoja ilikuwa Februari 14, 2026, ambapo iliifunga Namungo mabao 3-2.
Katika mchezo wa kesho utakaochezwa katika Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam, watakutana na Wekundu wa Msimbazi, ambao hawajafungwa kwenye mechi 10 za Ligi za hivi karibuni (wameshinda sita na sare nne).
Aidha, katika mechi 10 za Ligi walizokutana na Simba hivi karibuni, Prisons wameshinda moja, wamepata sare moja na kufungwa mara nane.






