WAZIRI WA IRAN AINYOOSHEA KIDOLE MAREKANI

Date:

Share post:

TEHRAN, Iran

NI Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ambaye ameitupia lawama Marekani akisema imekuwa ikitibua jitihada zote za kidiplomasia za kumaliza mgogoro uliopo kati ya mataifa hayo.

Wakati huo huo, Araghchi ameeleza kuwa Iran haitoendeshwa na presha inayopewa na Marekani, akilenga mashambulizi yanayoendelea katika Mlango-Bahari wa Hormuz.

Licha ya meli zinazopita katika Mlango-Bahari huo kuendelea kushambuliwa kwa mabomu, Rais Donald Trump amedai bado makubaliano ya kusitisha vita yanaheshimiwa.

Tayari Serikali ya Marekani imepeleka mapendekezo yenye kurasa moja kwa Iran juu ya kumaliza vita, kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani, Marco Rubio.

Iran inadhibiti Mlango-Bahari wa Hormuz, wakati huo pia Marekani ikiwa imepeleka wanajeshi wake eneo hilo kwa ajili ya kuzilinda meli zinazokatiza.

Mlango-Bahari huo ni eneo nyeti katika uchumi wa dunia kuwa asilimia 20 ya mafuta hupita hapo kwa usaifiri wa meli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MLANGO-BAHARI WA HORMUZ UNAVYOITESA DUNIA

TEHRAN, Iran MGOGORO unaoendelea kati ya Iran na Marekani katika Mlango-Bahari wa Hormuz umetikisa uchumi wa dunia. Kila nchi,...

MWAKA MMOJA WA PAPA LEO AKIIONGOZA VATICAN

WASHINGTON DC, Marekani UMETIMIA mwaka mmoja tangu Papa Leo XIV alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki duniani. Aliingia madarakani Mei 8,...

STEVE BARKER AMEANZA KUJIPATA LIGI KUU BARA

UKIFUATILIA msimamo wa Ligi Kuu Bara na kiwango cha Simba katika mechi za hivi karibuni, unaweza kusema sasa...

FEI TOTO KUVUNJA REKODI YA MIAKA MINNE LIGI KUU BARA?

TANGU George Mpole alipotwaa tuzo ya Mfungaji Bora Ligi Kuu Bara mwaka 2022, hakuna mchezaji mzawa aliyeweza kufanya...